Kocha kutoka Marekani Jonathan Markowitz akiwafundisha mchezo wa Rugby wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam katika tamasha la michezo lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.
Kocha kutoka Uingereza Ben Illingworth akiwafundisha mchezo wa Rugby wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam katika tamasha la michezo lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.
Wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam wakiwa katika tamasha la michezo ya Rugby kuendeleza mchezo huu Tanzania na lilohusishwa na Bhubesi Pride kutoka Uingereza, lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mnawapotezea muda vijana wetu, Ragbi waachieni India na Pakstani. Wafundisheni kandanda ndiyo inauzika kwetu!

    ReplyDelete
  2. kula tano mdau. Rugby na TZ wapi na wapi.rugby ni ya ulaya ambapo watoto wanaendeleza kipaji hadi ukubwani. hiyo danganya toto ya siku 1 inawasaidia nini? Wafundisheni watoto michezo kama long jump,high jump, track and field ili waweze kushiriki kwenye mashindano ya olympics. sasa hapo kupotezeana muda tu.watoto wenyewe hata viatu hawajavaa,rugby gani bila viatu. mweh,,. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Nadhani wadau #1&2,

    Ni vizuri kuwafungulia watoto milango ya vitu mbali mbali. Siyo mpira wa mgiuu pekee yake ndiyo uchezwe kwa vile una soko. Mie mwenyewe Mmbogo mwalimu wa mpira wa miguu, lakini naelewa umuhimu wa watoto wetu kujifunza michezo mbali mbali kwani sio kila mtu ana kipaji cha kucheza mpira. Inatakiwa kuwe na michezo kibao, na kama tumepata watalaamu wa Rugby ingawa ni siku moja ni sawa tu,kwani wanawafungua watoto macho kwenye michezo mipya. Mtoto mwenyewe akipenda mchezo fulani anaweza akafuatilia na kuendeleza kipaji chake, mfano nani alijua Hasheem angeweza kuchezea NBA?! Huku Ughaibuni watoto wanacheza michezo mbali mbali wakiwa watoto, na sana soka, baadaye wanacheza basketball au American Football. Mfano, Candace Parker-mchezaji bora basketball Marekani nzima alikuwa akichezea soka kwenye timu yangu alipokuwa mdogo, lakini baadaye akamua kucheza basketball.

    ReplyDelete
  4. mdau wa juu umekusudia cricket nini sijawahi kusikia wadosi wakicheza rugby maana mchezo huu ni noma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...