Na Mwandishi Wetu
Jumla ya warembo 16 wametemwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Tabata ambao utafanyika Mei 31 Dar West Park.
Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana kuwa warembo hao wametemwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, kukosa sifa za kushiriki na utovu wa nidhamu.
Kalinga aliwataja warembo waliyotemwa kuwa ni Sophia Claud (21), Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Ray Issa (22), Shamim Abass (22), Shan Abass (22), Amina Ally (18), Magdalena Bhoke (21)  na Zilpha Christopher (19)
Kalinga aliwataja warembo wanoendelea na mazoezi katika umbumbi wa Dar West Park, Tabata kila siku kuwa ni Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20) and  Glory Jigge (18).
Wengine ni Rachel Mushi (20), Caroline Sadiki (20), Kabula Juma Kibogoti (20), Blath Chambia (23), Suzzane Daniel Gingo (18), Upendo Lema (22), Pasilida Mandari (21) na Martha Gewe (19).
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Redds Miss Tabata inaandaliwa na  Bob Entertainment na Keen Arts na chini ya Udhamini wa Redds, CXC Africa, Fredito Entertainment, Brake Point, Michuzi Media Group na Saluti5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Uzuri wa Mkakasi ndani ganda la mti:

    Ama kweli Urembo hauishii kwenye uso tu bali ni kulinga na Tabia na mwenendo!

    Yaani Mabinti ile tu Mchakato wa kuandaliwa kushindania Taji haujakamilika tayari mmemwagwa!,,,inaonyesha ni jinsi gani ambavyo hamuwezi kuwa Kigezo chema ktk jamii kwa Utovu wa Nidhamu na Kasoro nyinginezo.

    Bora mmemwagwa na mapema labda tungepata Mwakilishi asiyestahili matokeo yake tukajuta baadae baada ya Muhusika kushindwa kuwajibika ktk Jamii.

    Inawezekana kabisa kwa kasoro hizo mkawa pengine pia baadae mkawa Hamuoleki!

    Ama kweli Kunguru hafugiki!

    ReplyDelete
  2. Sometimes waandazi wakinyimwa yale mambo yetu, wanaamuwa kufanya maamuzi ya kuwakomowa hawa mabinti. Pumbafu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...