Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua Jambo wakati alipotembelea Mradimpunga wa Umwagiliaji kwenye Bonde la Mpunga la Jendele kulia Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa waziri alifanya Ziara ya Wilaya ya Kati Unguja kukutembelea Mradi Uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipita kwenye shamba la mpunga la kuzalishia Mbegu la kinyasini-kisongoni Walaya ya Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika Ziara ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na ASSP. Picha na Ali Meja.


Na Ali Issa, Maelezo, Zanzibar
Waziri wa nnchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe Samia Suluhu Hassan amesema  kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kuituza na kuindeleza miradi inayo fadhiliwa na Serikali zote mbili  na washirika wa maendeleo ili miradi hiyo iendelee kuwanufaisha na kutimiza lengo lililokusudiwa.

Hayo ameyasema huko Jendele wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipo fanya ziara  kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo iliyofadhiliwa na TASAF kupitia Serikali ya Muungano wa Tanzania.

Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wananchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwalengo kwamba wananchi hao waweze kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato jambo ambalo baada ya mradihuo kukabidhiwa wananchi husuasua na hatimae kufa kituambacho hakifurahishi.

Amesema wana nchi wajifunze kuituza na kuendeleza miradi hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufahisha wao wenyewe. “Kuiacha miradi ife si vizuri. Muichangie iliijiweze kujiendesha na hiyo ndiyo faida ya miradi hiyo”.alisema Samia.

Aidha Waziri aliwambia wakulima wa bonde la Jendele, Kinyasini na  Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu kwavile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo  uzalishaji ungezeke.

Waziri huyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyo tumika katika miradi ilio ombewa na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi. Alifurahishwa na juhudi zinazochukuliwa kwani kumefikiwa hatua kubwa za kumaendeleo na zinatia moyo kwa matumaini .

Waziri alitembelea mradi wa  mpunga wa umwagiliaji maji jendele na mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga Kinyasini na Kisongoni na baadae kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL inayo endeshwa na wizara yakilimo na maliasili na ushirika Zanzibar .

Miradi hiyo kwa TASAF ya awamu ya kwanza Zanzibar   ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu ambapo ziligawiwa sawa sawa kwa Unguja na Pemba.

Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani 2,500.000.00  ambapo zilitumika kumalizia mradi wa kwanza Unguja na Pemba kupitia  mfuko wa Taifa wa kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00

Ziara hiyo itaendelea kwa  kutembelea idara ya uhamiaji Zanzibar na malaka ya kitambulisho cha Taifa Zanzibar.  






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nimekuvulia kofia mama, kweli wewe kiongozi hata tope hujali!

    ReplyDelete
  2. Hawa ndo kati y viongozi wachache tulionao ambao hawajitangazi lakini wako committed.
    Big up mama!!!

    ReplyDelete
  3. Nashukuru sana Mama kwa mfano wako mzuri. Hawa ndiyo Mawaziri tunaowataka sisi Watanzania. Wenye kujituma kwenda kule wanakoishi Watanzania halisi wanaohitaji kusaidiwa.

    Mwenyezi Mungu na azidi kukupandisha Mama yangu.

    ReplyDelete
  4. kwani hakujua kuwa atakutana na kaka/dada tope?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...