Badhi ya Abiria wakiwa kituo cha mabasi mjini Lindi
bila kuelewa hatma ya safari yao hii leo.
baadhi ya mabasi yaendayo mtwara yakiwa mjini Lindi toka
jana baada ya mgomo huo kuhofia usalama.
Mmoja wa Madereva wa Mabasi akiongea na waandishi wa habari.
KAMANDA wa Polisi mkoa wa Lindi George Mwakajinga akiwasihi
madereva kuridhia kusindikizwa na polisi kwenda mtwara.
Askari Polisi wakiwa tayari kwa ulinzi na kuyasindikiza mabasi hayo mpaka mkoani Mtwara.
Na Abdulaziz Video - Globu ya Jamii,Lindi
Zaidi ya Abiria 400 Waliokuwa wanafanya safari kati ya Dar es salaam na Mtwara
jana wamelazimika kusitishiwa safari mkoani Lindi kufuatia madereva na
wamiliki wa Mabasi waliyokuwa wanasafiria kuogopa kutokana na hali ya
Amani kutokuwepo Mkoani Mtwara kufuatia Vurugu za Mgogoro wa Gesi.
Ripota wa Blog ya jamii alifika katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Lindi na
kukuta msongamano Huo ambapo Jeshi la Polisi Mkoani Lindi likiongozwa
na kamanda wa Polisi wa Mkoa,George Mwakajinga Likitoa ulinzi
kwa mabasi hayo kuyafikisha Mtwara hali ambayo imekataliwa na Madereva
wa Mabasi pamoja na baadhi ya Abiria.
Kamanda Mwakajinga akiongea na blog hii alieleza kuwa sambamba na
kuhakikishiwa Usalama wa mabasi hayo kwenda Mtwara alishangazwa na
baadhi ya madereva kugoma kusindikizwa na Polisi kwa hofu ya Usalama
wa Magari na Abiria wanaowasafirisha.
Mwandishi hakika Jeshi limejipanga kuwasindikiza hadi mtwara ila
nimepigwa na butwaa baada ya abiria na Madereva kugoma kwenda mpaka
sasa sijui tufanye nini maana sasa ni mgomo huu ila nakuhakikishia
bado tutawapa Ulinzi wa Kutosha na watakuwa salama.
Baadhi ya Madereva wa Mabasi hayo walieleza hofu yao kuhusu kuendelea
na safari huku baadhi ya Abiria wakiwa na misimamo Tofauti kuhusiana
na Hali hiyo Ambapo wengine wanalazimishwa kusafiri wengine wakihofia
usalama wao huku madereva wakikataa kuondoka Lindi.
Asubuhi Mmiliki wa Basi la Buti la Zungu,Zubeiry Namachokole ameamua
kutoa gari yake nyingine aina ya Coaster kuwapeleka abiria wake
waliolala Lindi badala ya Basi yake ya Yutong kuhofia usalama wa Basi
hilo.
Hadi tunakwenda Mitamboni abiria wengi walikuwa wakihangaika kwa
makondakta na Madereva huku wakitafuta msaada wa Serikali ili
wasaidiwe chakula na hifadhi hadi hali itakaporejea kuanza safari
kutokana na wengi kusafiri wakiwa na hali ngumu wakiwemo akina mama na
watoto
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...