Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) na kushoto risasi moja kama kionekanavyo kioo cha juu,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.
Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.
Mmoja wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali),mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    nadhani hizo pesa zimekuwa raced pahala si bure check ramani ilipotoka hizo pesa mpaka anakoelekea kwani walijuaje kuwa hilo gai lina pesa hicho?

    Hakuna tofauti kati ya ile issue ya Ada Estate wachina walipoibiwa mshahara wa wafanyakazi hao...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    walipewa mchoro tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Mhmmmmm si bure huo mchongo wa watu wa macounter benki jamaa akichukua wanaripoti na watakuwa na watu wao walioko karibu na hapo wanashutuliwa!! wazeni mbali jamani mambo yamekuwa mabaya sio mpaka mtu wa nje.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    Mtu keshauza lada hapa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2013

    Inatisha. Namna hii tutafika kweli jamani?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2013

    Kuna haja ya wizara husika kuangalia namba ya kuwa na mashine za wafanyabiashara kupokea na kufanya malipo kwa soft-money. Hapa Africa ya kusini unaweza kuishi mwezi mzima bila kuiona noti na ukalipa kwa kadi ya benki,hii inapunguza sana mambo ya kuuana kwa ajili ya pesa na pengine hata siyo pesa zako mwenyewe. Hii itasaidia, mfano ukiwa na eldu 5 au 20 tu za matumizi nani ataharibu risasi zake kwa hela hiyo,sana sana vibaka watachukua,utasikitika ndio lakini utakuwa salama.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2013

    We need to arm all of the police men with hand guns ,if this trooper had a hand gun with him he would have fought back and serve the victim

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2013

    Watu sasa waache kubeba cash kubwakubwa kama hizi watumie transfer za kibenki itapunguza sana matukio kama haya. Inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2013

    hilo dili

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2013

    Kweli Tanzania si mahali pa kuishi. It's all inside job. Kila mtu mtu anataka kutajirika hata kwa kutoa mtu roho.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2013

    Duh, tz tulipofikia? Kuna haja ya kuwa na cctv kwenye mataa.. Poor him...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2013

    kiukweli njaa itatuumiza tisipoangalia. Huu mchongo umefanywa na mtu wa karibu au pesa zilipochukuliwa maana siku hizi watu wa mabenki wanamitandao yao wakijua unachukua pesa nyingi wanapanga mikakati. enyi wafanyakazi wataasisi za fedha kuweni na maadili kumbukeni unachofanya leo kwa mwenzio kesho kwako au kwa ndugu yako wa karibu. Polisi waanzie pale pesa zilipotoka.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2013

    Kama hilo gari limetokea bank hiyo bank ishikwe shati kabisaa. Vitendo kama hivi vimekuwa vikitokea sana wafanyabiashara wanapotoka bank!! Inabidi serikali imyaanya'anye leseni hizo bank husika kabisa!!! lazima hiyo ni inside job mia ya mia!

    ReplyDelete
  14. Uchunguzi ni lazima uanzie hukoooooo bank!! Or huyu mtu hakutokea bank??? Or ni deal limekwenda vibaya

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2013

    Wazee wa kazi wamechukua chao. Inabidi sasa jamii ibadilike hatuwezi kuendelea kutembea na magunia ya noti lazima tupate njia mbadala ya malipo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2013

    so sad jamani

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 24, 2013

    inabidi iitwe FBI hapa kufanya uvhunguzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...