Mechi ya Fainali kugombea kombe la Mbuzi na jezi kati ya Manunda FC na G-West iliyofanyika kwenye Uwanja wa Msisiri A Jana 12/5/2013 Mwananyamala DSM ilikua na vimbwanga vya aina yake ambapo moja ya tukio la kukumbukwa ni pale timu hizo zilipokataa katakata kubadili jezi zilizokuwa zikilandana kwa madai kwamba tayari zilishapitia kwa "Babu" Licha ya Jitihada ya mwamuzi na watu wenye ushawishi, hakuna timu iliyokubali na hivyo mwamuzi akalazimika kuchezesha mechi hiyo ya mchangani kwa matakwa ya timu hizo
Mechi hiyo iliishia kwa G West kuibuka mabingwa kwa njia ya Penalty 4-2 baada ya dakika za kawaida kuisha kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1, wafungaji wakiwa na Msimbe kwa Manunda dk ya 43 na Mome dk ya 81

Matukio mengine yaliyogubika mechi hizo ni wachezaji wawili wa G-West kuanguka uwanjani kwa imani za kuzidiwa na majini, pamoja na washabiki kuvunja nazi na mayai kwa imani za ushirikina na G-West kunyweshwa maji yaliyochanganywa na majani mithili ya Alovera badala ya maji ya kawaida  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2013

    Da nakumbuka home na kitambo sana wakati huo na washkaji tukiangalia mashindano ya mchangani kwa sana maeneo kama mwananyamala B shuleni,Magomeni(Refa Tindwa),Tandale maguniani,Abajalo sinza,Mwananyala kopa, kijitonyama uwanja wa bora.Ilikua burudani tosha, nakumbuka miaka hiyo kulikua na masela wa kila timu na siku zote mwishoni lazima moto uwake(ngumi).

    ReplyDelete
  2. Geofrey ChambuaMay 14, 2013

    uko wapi mkuu, unapokumbuka muwe pia mnakumbuka hali za wachezaji wetu hapa bongo, ona hawa hawana viatu na mpira wa makaratasi, na ni watu wazima kabisa
    Kweli inakumbusha mbali sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2013

    picha imenivutia sana hizi, imani hizi bado zipo bongo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2013

    jamaa kweli wako peku kabisa

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2013

    jamaa mwenye msuli anaonekana ndiye kabeba mikoba

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2013

    hii inafaa kupelekwa TFF waone jinsi ya kusupport hao vijana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...