Mechi ya Fainali kugombea kombe la Mbuzi na jezi kati ya Manunda FC na G-West iliyofanyika kwenye Uwanja wa Msisiri A Jana 12/5/2013 Mwananyamala DSM ilikua na vimbwanga vya aina yake ambapo moja ya tukio la kukumbukwa ni pale timu hizo zilipokataa katakata kubadili jezi zilizokuwa zikilandana kwa madai kwamba tayari zilishapitia kwa "Babu" Licha ya Jitihada ya mwamuzi na watu wenye ushawishi, hakuna timu iliyokubali na hivyo mwamuzi akalazimika kuchezesha mechi hiyo ya mchangani kwa matakwa ya timu hizo
Mechi hiyo iliishia kwa G West kuibuka mabingwa kwa njia ya Penalty 4-2 baada ya dakika za kawaida kuisha kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1, wafungaji wakiwa na Msimbe kwa Manunda dk ya 43 na Mome dk ya 81
Matukio mengine yaliyogubika mechi hizo ni wachezaji wawili wa G-West kuanguka uwanjani kwa imani za kuzidiwa na majini, pamoja na washabiki kuvunja nazi na mayai kwa imani za ushirikina na G-West kunyweshwa maji yaliyochanganywa na majani mithili ya Alovera badala ya maji ya kawaida


Da nakumbuka home na kitambo sana wakati huo na washkaji tukiangalia mashindano ya mchangani kwa sana maeneo kama mwananyamala B shuleni,Magomeni(Refa Tindwa),Tandale maguniani,Abajalo sinza,Mwananyala kopa, kijitonyama uwanja wa bora.Ilikua burudani tosha, nakumbuka miaka hiyo kulikua na masela wa kila timu na siku zote mwishoni lazima moto uwake(ngumi).
ReplyDeleteuko wapi mkuu, unapokumbuka muwe pia mnakumbuka hali za wachezaji wetu hapa bongo, ona hawa hawana viatu na mpira wa makaratasi, na ni watu wazima kabisa
ReplyDeleteKweli inakumbusha mbali sana
picha imenivutia sana hizi, imani hizi bado zipo bongo?
ReplyDeletejamaa kweli wako peku kabisa
ReplyDeletejamaa mwenye msuli anaonekana ndiye kabeba mikoba
ReplyDeletehii inafaa kupelekwa TFF waone jinsi ya kusupport hao vijana
ReplyDelete