JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA
   

    WIZARA YA MAJI 






              TAARIFA KWA UMMA

Katika gazeti la Nipashe la Jumapili tarehe 12 Mei 2013 mwandishi Mashaka Mgeta aliandika makala yenye kichwa cha habari “Aibu kwa Profesa Maghembe na dharau kwa wataalamu wa Wizara” na kuwa, Wizara ya Maji imejiwekea rekodi chafu kwa bajeti yake kurejeshwa kabla ya kupitishwa na Bunge na wataalamuwa wa Wizara ya Maji wamekuwa miongoni mwa wasiosikilizwa na kupuuzwa suala hilo si la kweli.
Mnamo tarehe 24 na 25 Aprili, 2013, Waziri wa Maji Mhe. Prof. Jumanne  Abdallah Maghembe (MB) aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014. Bajeti hiyo iliwasilishwa na mjadala uliendelea kwa muda wa Siku mbili. 
jadala mkubwa ulikuwa Bungeni baada ya kuwasilisha maoni ya Kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa Bajeti ya Wizara ya Maji haitoshi.
Mjadala ulihairishwa na Mhe. Spika chini ya Kanuni ya Bunge 67(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kama Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 2 Toleo la 2002.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2013

    Jamani mkianza kujibizana na tabloids mtafika pabaya dawa ya tabloid ni kuidharau na kuchapa kazi. Wananci wakiridhika na huduma za serikali, tabloid haitakuwa na nafasi ya kutusamaratisha. Tatizo la wizara ya maji ni kuwa hamtaki kupanua huduma, kukarabati maboma na kuongeza sehemu za kuhifadhia maji kwa capacity na idadi. Mkifanya hivyo, na wenzenu wa umeme wakiacha kutukatia umeme wala hatutajali yanayoandikwa na magazeti yenye nia ya kuichafua serikali na nchi nzima.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Hata mimi kidogo nilishangaa na hiyo statement ya Bwana Mashaka Mgeta. Bajeti ya Wizara ya Maji huwa inaathirika kama hizo za Wizara nyengine.

    Ceiling ya bajeti huwa wanapangiwa na Wizara ya Fedha, na nyongeza nyengine yo yote lazima iidhinishwa huko.

    Kwa hivyo kuisema Wizara kama Wizara wala haina mantiki yo yote.

    Nilidhani Bwana Mgeta anayaelewa haya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...