Lori la kampuni ya Mafuta ya Lake Oil likiwa limepata ajali maeneo ya Mlima Nyoka-Mkoani Mbeya,Aidha katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha isipokuwa baadhi ya watu kadhaa walijeruhiwa.
 Baadhi ya Wakazi kutoka maeneo mbalimbali ya Mlima Nyoka ikiwemo jirani na mji maarufu wa kibiashara,Uyole jijini Mbeya wakiwa wamejumuika kwa pamoja wakigombea mafuta yaliyokuwa yakimwagika,mara baada ya Lori la Lake Oil kupata ajali.Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2013

    Hahahahaha hahahaha hahahahah ahhahhahaha hahahaha mbeya mbeya mbeya mbeya, yaonesha safari hii walikua makini sana kwani walijishughurisha na mafuta tu na si kuchomoa betri tena, hahahahaha hahahaha wamejifunza kidogo,

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2013

    Yale yale watu hawakomi hawafikirii kufa....utadhani hawasikilizi habari .... akili zao zinakuja saa sita usiku.... watu wengi wamekufa kwa kukimbilia magari ya mafuta yaliyopata ajali.... hawafikiri kitakacho weza kutokea. Jamani hatakama ni umasikini sio hivyo....hali hiyo mpaka lini jamani?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2013

    Hawa watu hawajui kama wanalichezea bomu? Likilipuka hapo hakuna cha salia mtume!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2013

    mikono ya mwenye njaa haisubiri kunawa wakati chakula kinapopatikana....Viongozi wetu wanatutia umaskini sio makosa ya waongozwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2013

    Sema genge la wezi wa mafuta ktk gari lililopinduka

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2013

    Uza roho baba usijali kufa kwani mwisho wa maisha ya duniani ni kifo tu. No any other alternative.Kumba mafuta hayo ya bwerere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...