Na Abdulaziz Video,Kilwa 
MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi  Mhe. Abdalah Ulega ameonya kuwa hatakuwa na msamaha kwa mzazi yeyote atakayeshindwa kumpeleka mtoto wake kuanza kidato cha kwanza kwa kisingizio cha umaskini wa kipato. 
Akizungumza katika mahojiano na Globu ya Jamii ofisini kwake, Mkuu huyo wa wilaya amesema kumekuwa na visingizio vingi kutoka miongoni mwa wazazi wanapohimizwa kuwapeleka watoto wao shule kwa madai kwamba hawana uwezo. 
''Ukiwafuatilia watoto utasikia wazazi wanaanza utetezi Sina Uniform,Sina ada mara viatu na visababu vingi hii mwandishi siwezi kuliachia watoto hawa wataishi vipi baadae Wapo wakuu wa wilaya,madaktari,walimu wa baadae kwa nini tuwasitishie maisha yao...
"Hii siwezi kukubali na Nimeagiza na si kuagiza tu nitafuatilia kuhakikisha watoto wanaelimika' Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa endepo katika familia kutakuwepo na mzazi hasiye jiweza, kinachotakiwa ni kuchukua hatua ya kumpeleka mtoto wake shuleni kwanza na kwamba mambo mengine yakiwemo ya ada na sare ya mwanafunzi yataendelea kutekelezwa taratibu wakati mwanafunzi akiendelea na masomo.
''Sasa Kilwa Inapata mrahaba wa gesi ya songosongo takriban Milioni 100 na hivi karibuni mambo yakienda vizuri Halmashauri itakuwa inaingiziwa Karibu milioni 300 kutokana na gesi kwa mwezi na Wakubwa Madiwani wamepitisha kupitia baraza la madiwani kuwa mapato hayo aslimia 35 iende katika kuboresha elimu
"Je nikiacha raslimali za Kilwa zitachukuliwa na wageni wenyeji wakiwa watumwa...Kwa hili wazazi nitaenda nao sambamba na timu yangu ipo imara...Alimalizia Ulega.
 Sambamba na hayo ilibainika kuwa hadi kufikia juma lilopita, jumla ya wanafunzi 414 wakiwemo wavulana 316 wasichana 98 waliochaguliwa kuingia kitado cha kwanza mwaka huu walikuwa bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi  Mhe. Abdalah Ulega wakati wa mahojiano haya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Wewe kama kiongozi unatakiwa kuja na solution kwa wazazi wasiokua na uwezo na sio kuwatishia. Je wakiwapeleka shule kwanza bila sare na ada hapo baadae ikiwa bado hawana uwezo wa kuzilipia je utawafunga? mimi nilifikiria unayo mawazo ya maana ya kuwasaidia hao wazazi wasiokua na uwezo. hayo mapato ya gesi ambayoutayapata sio wewe kutoa amri vipi itumike, ila ni wananchi ndio wapange kipi wanakihitaji ili hizo fedha zi wasaidie.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Kijana huo ukuu wako wa wilaya utakufikisha pabaya huko ni kilwa,utajikuta unaamka baharini kila siku,hapana chezea hao watu wa pwani,kuna mkuu wa mkoa aliwapa amri wazee Lindi alijukuta yuko beach na taulo aliomba kuama mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2013

    Unaapa! Si bora ungetumia neno jepesi UNAAHIDI. Kiapo ni neno zito endapo hutokitimiza kile ulichokiapia kukitekeleza, japokuwa pia ahadi ni deni, lakini inaweza kutimizwa japo sio leo hata mwakani na pengine isikamilike vyema ukilinganisha na kitu ulichokiapia kukitekeleza. Tujaribu kuwa makini na kauli zatu zisije kukufikisha tusipostahili. Kila la kheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...