Maandalizi yanafanyika kwa ajili ya kuwakutanisha wale waliosoma Shule ya Mkwawa, Iringa kuanzia mwaka 1965 hadi 2005 kabla ya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Mkwawa University College of Education (MUCE)

Siku: Jumamosi 22 Juni, 2013
Mahali: Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (mkabala na IFM)
Mchango: Shilingi elfu hamsini (50,000/-) @ mtu


Mchango huu ni kwa ajili ya kugharamia matangazo katika vyombo vya habari, vinywaji, chakula, ulinzi, mapambo, kukodi viti na meza, mshereheshaji (MC) na PA, live band. Tiketi zitapatikana wiki moja kabla ya siku ya shughuli

Shughuli hii itakuwa ni mwanzo wa kuchangia Chuo cha Elimu Mkwawa (MUCE) ili kuweza kujenga mabweni (hostels) kwa ajili ya wanafunzi

WanaMkwawa tuko wengi na tuna kila fursa ya kujumuika pamoja kukumbushana ya Makongoro na Magembe, Makanyagio na Lumumba, Aggrey na Shaaban Robert!

MUCE wamefungua portal kwa ajili ya Mkwawa Alumni tafadhali jisajili ili kuwa sehemu ya familia kubwa ya Mkwawa http://muce.ac.tz/index.php/alumni-registration

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Kamati ya Maandalizi kupitia: Catherine David
Email: Cathyjeff2001@yahoo.com
Simu: +255 784/15 609 848
Mkeka wa Nguvu kuingia Iringa mjini.
Bustani ya Garden katika  Shule ya Mkwawa, Iringa.
Wadau wakipata msosi enzi hizooo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    Chuo sisi ndo tukijengee mabweni. Kodi inayokusanywa na serikali inakwenda wapi? Kama ni kukutana kupanga utaratibu wa kuanzisha miradi yetu kwa ajili ya maisha yetu sawa. Lakini kwenye ujenzi wa mabweni mimi simo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2013

    Joel kalanje kaka mkuu atakuepo Jamani

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2013

    Wadau je ktk Picha ya chini wakipoata msosi ilikuwa ni mwaka gani?

    Kitu kizuri ktk kutoka Maktaba ni kupata na mwaka tukio lilipofanyika ili tuweze kuvuta taswira kutoka siku hizo hadi leo ilivyokuwa.

    Pana raha yake kuvuta kumbukumbu sambamba na miaka saaana!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2013

    Hapo naona umechemsaha Bustani ya GARDEN!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2013

    Nawatakia kila la heri. Nilisoma hapo mwaka 1974-75. Ningejiunga na nyie, kwa bahati mbaya nilishahama Tanzania miaka mingi!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2013

    Nakumbuka maandazi ya Makanyagio! Du makuuuuuuubwaaaaaaaaa! yalikuwa!
    I wish I could be there!
    I will be hone in two years by Grace of God, so may be next meeting I can join you guys.
    INSH ALAH

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2013

    Halafu CDM wanasema ndani ya miaka 50 hakuna kilichofanyika...jamani kweli?

    ReplyDelete
  8. Yale yale ya "BARABARA ya Bagamoyo ROAD" ndio yaliyojitokeza na hapo kwenye hiyo picha ya tatu "BUSTANI ya GARDEN katika Shule ya Mkwawa, Iringa." Kweli Kiswahili ni lugha yetu lakini mmh! Hata kama ni 'code mixing' basi siyo hivyo. Tujitahidi katika matumizi fasaha ya lugha na hasa kwenye uandishi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2013

    Mtoa Maoni wa 5:
    -----------------------------------'''Nawatakia kila la heri. Nilisoma hapo mwaka 1974-75. Ningejiunga na nyie, kwa bahati mbaya nilishahama Tanzania miaka mingi!'''
    -----------------------------------

    Kweli ndugu yetu umechelewa!

    Kama umehama Tanzania JE SASA ULIKOHAMIA UPO SAYARI GANI?

    Kama hijasikia pana kitu kinaitwa Diaspora Community, ni kuwa Asili ya mtu HAIKWEPEKI HATA KAMA UTAKUWA SAYARI GANI 'MFANO HUKOULIPO ANGALIA KWENYE REKODI ZAO WANAVYOKUTAMBULISHA NI KUWA UNA ASILI YA TANZANIA, HATA KAMA WATAKUPA PASIPOTI ITAANDIKWA UNA ASILI YA TANZANIA.

    HIVYO HUWEZI KUTUPA JONGOO NA MTI WAKE UNA NDUGU ULIOWAACHA NYUMA HUKU TANZANIA, UNAWEZA KUSHIRIKI KUPITIA DIAPSORA COMMUNITY.

    Dunia imeshuhudia Jamii Kongwe za Madiaspora kama:

    1.WAYAHUDI, kokote walipo lakini bado wanajihesabu kama sehemu ya Taifa la Israel.

    2.WAHINDI, vilevile ni Madiaspora wakongwe duniani, hadi unaowaona hapa Tanzania.

    3.WAARABU, vilevile.
    4.WASOMALI, ambao hata hapawakipewa Pasipoti wanakuwa hawaaminiki kama Raia wengine huwa wanapewa Namba za Mafaili zinazoitwa KSA, hii yote ni kwa sababu kila Msomali popote alipo abu kama sehemu ya Taifa la Somalia.

    5.WATANZANIA: Pamoja na WEWE MWENYEWE HUKO ULIPO nao ni Madiaspora wakongwe sana Duniani wametapakaa nchi nyingi sana wakiwa wameingia huko miaka mingi iliyopita.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2013

    Mtoa Maoni wa TANO,

    Inaonyesha hupitii hii kitu anayotoa Ankali kila siku humu ,MKATAA KWAO NI MTUMWA !

    Kwa kauli yako hiyo 'NILIISHA HAMA TANZANIA SIKU NYINGI' na hiyo Pasipoti yako ya Sweden sijui Norway INAKUPA KIBURI inaonyesha hata kama ukiisikia Lizombe ama Mdumange ngoma ya kwenu utajifanya hujui kuucheza kisa una Uraia wa Sweden!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2013

    No.5 umechemsha!

    Huko uliko hata kama watakupa Pasipoti ni lazima wataandika umezaliwa LUDEWA-IRINGA!

    Hivyo huwezi kukana kwenu.

    Unaweza kuhama kwenu moja kwa moja?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2013

    Naunga mkono hoja ya mjumbe wa kwanza kabisa!....mimi nalipa P.A.Y.E kila mwezi bila kutegea na sipo legelege katika kulipa hata kidogo!, sasa wahusika ulegelege wanautoa wapi?. Yaani nakataa kubebeshana mizigo iliyo/inayotokana na kukosa umakini kwa kundi fulani.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 30, 2013

    Njaa kali huleta wivu, na wivu unaua.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2013

    YAANI JAMANI PICHA KAMA ZA WAFUNGWA VILE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2013

    hii picha itakuwa kati ya mwaka 1997 na 1999, namuona Safiniel Mbaga maskini RIP dada, huyu wa kwanza ni Denis ALfred nadhani yuko BOT

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2013

    RIP SAFINIEL, NILIKUWA NAE CLASS MOJA 1997-1999, nyambari nyangwine, peter kibatala, we riziwan,hassan mwemweta, kakere celestine, mtoroki majaliwa, irene kiwia, sundi fimbo and many more msikose!
    hi mtoa taarifa, basi fafanua zaidi ili watu wajipange c unajua time is money? muda ni saa ngapi? na kama wanachangiwa MUCE iweje walionza 2005 wasihusishwe ilhali ndio haswa watatueleza ugumu wa mazingira toka kiwe chuo kikuu kishiriki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...