Maandalizi yanafanyika kwa ajili ya kuwakutanisha wale waliosoma Shule ya Mkwawa, Iringa kuanzia mwaka 1965 hadi 2005 kabla ya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Mkwawa University College of Education (MUCE)
Siku: Jumamosi 22 Juni, 2013
Mahali: Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (mkabala na IFM)
Mchango: Shilingi elfu hamsini (50,000/-) @ mtu
Mchango huu ni kwa ajili ya kugharamia matangazo katika vyombo vya habari, vinywaji, chakula, ulinzi, mapambo, kukodi viti na meza, mshereheshaji (MC) na PA, live band. Tiketi zitapatikana wiki moja kabla ya siku ya shughuli
Shughuli hii itakuwa ni mwanzo wa kuchangia Chuo cha Elimu Mkwawa (MUCE) ili kuweza kujenga mabweni (hostels) kwa ajili ya wanafunzi
WanaMkwawa tuko wengi na tuna kila fursa ya kujumuika pamoja kukumbushana ya Makongoro na Magembe, Makanyagio na Lumumba, Aggrey na Shaaban Robert!
MUCE wamefungua portal kwa ajili ya Mkwawa Alumni tafadhali jisajili ili kuwa sehemu ya familia kubwa ya Mkwawa http://muce.ac.tz/index.php/alumni-registration
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Kamati ya Maandalizi kupitia:
Catherine David
Email: Cathyjeff2001@yahoo.com
Simu: +255 784/15 609 848
Mkeka wa Nguvu kuingia Iringa mjini.
Bustani ya Garden katika Shule ya Mkwawa, Iringa.
Wadau wakipata msosi enzi hizooo
Chuo sisi ndo tukijengee mabweni. Kodi inayokusanywa na serikali inakwenda wapi? Kama ni kukutana kupanga utaratibu wa kuanzisha miradi yetu kwa ajili ya maisha yetu sawa. Lakini kwenye ujenzi wa mabweni mimi simo.
ReplyDeleteJoel kalanje kaka mkuu atakuepo Jamani
ReplyDeleteWadau je ktk Picha ya chini wakipoata msosi ilikuwa ni mwaka gani?
ReplyDeleteKitu kizuri ktk kutoka Maktaba ni kupata na mwaka tukio lilipofanyika ili tuweze kuvuta taswira kutoka siku hizo hadi leo ilivyokuwa.
Pana raha yake kuvuta kumbukumbu sambamba na miaka saaana!
Hapo naona umechemsaha Bustani ya GARDEN!
ReplyDeleteNawatakia kila la heri. Nilisoma hapo mwaka 1974-75. Ningejiunga na nyie, kwa bahati mbaya nilishahama Tanzania miaka mingi!
ReplyDeleteNakumbuka maandazi ya Makanyagio! Du makuuuuuuubwaaaaaaaaa! yalikuwa!
ReplyDeleteI wish I could be there!
I will be hone in two years by Grace of God, so may be next meeting I can join you guys.
INSH ALAH
Halafu CDM wanasema ndani ya miaka 50 hakuna kilichofanyika...jamani kweli?
ReplyDeleteYale yale ya "BARABARA ya Bagamoyo ROAD" ndio yaliyojitokeza na hapo kwenye hiyo picha ya tatu "BUSTANI ya GARDEN katika Shule ya Mkwawa, Iringa." Kweli Kiswahili ni lugha yetu lakini mmh! Hata kama ni 'code mixing' basi siyo hivyo. Tujitahidi katika matumizi fasaha ya lugha na hasa kwenye uandishi.
ReplyDeleteMtoa Maoni wa 5:
ReplyDelete-----------------------------------'''Nawatakia kila la heri. Nilisoma hapo mwaka 1974-75. Ningejiunga na nyie, kwa bahati mbaya nilishahama Tanzania miaka mingi!'''
-----------------------------------
Kweli ndugu yetu umechelewa!
Kama umehama Tanzania JE SASA ULIKOHAMIA UPO SAYARI GANI?
Kama hijasikia pana kitu kinaitwa Diaspora Community, ni kuwa Asili ya mtu HAIKWEPEKI HATA KAMA UTAKUWA SAYARI GANI 'MFANO HUKOULIPO ANGALIA KWENYE REKODI ZAO WANAVYOKUTAMBULISHA NI KUWA UNA ASILI YA TANZANIA, HATA KAMA WATAKUPA PASIPOTI ITAANDIKWA UNA ASILI YA TANZANIA.
HIVYO HUWEZI KUTUPA JONGOO NA MTI WAKE UNA NDUGU ULIOWAACHA NYUMA HUKU TANZANIA, UNAWEZA KUSHIRIKI KUPITIA DIAPSORA COMMUNITY.
Dunia imeshuhudia Jamii Kongwe za Madiaspora kama:
1.WAYAHUDI, kokote walipo lakini bado wanajihesabu kama sehemu ya Taifa la Israel.
2.WAHINDI, vilevile ni Madiaspora wakongwe duniani, hadi unaowaona hapa Tanzania.
3.WAARABU, vilevile.
4.WASOMALI, ambao hata hapawakipewa Pasipoti wanakuwa hawaaminiki kama Raia wengine huwa wanapewa Namba za Mafaili zinazoitwa KSA, hii yote ni kwa sababu kila Msomali popote alipo abu kama sehemu ya Taifa la Somalia.
5.WATANZANIA: Pamoja na WEWE MWENYEWE HUKO ULIPO nao ni Madiaspora wakongwe sana Duniani wametapakaa nchi nyingi sana wakiwa wameingia huko miaka mingi iliyopita.
Mtoa Maoni wa TANO,
ReplyDeleteInaonyesha hupitii hii kitu anayotoa Ankali kila siku humu ,MKATAA KWAO NI MTUMWA !
Kwa kauli yako hiyo 'NILIISHA HAMA TANZANIA SIKU NYINGI' na hiyo Pasipoti yako ya Sweden sijui Norway INAKUPA KIBURI inaonyesha hata kama ukiisikia Lizombe ama Mdumange ngoma ya kwenu utajifanya hujui kuucheza kisa una Uraia wa Sweden!
No.5 umechemsha!
ReplyDeleteHuko uliko hata kama watakupa Pasipoti ni lazima wataandika umezaliwa LUDEWA-IRINGA!
Hivyo huwezi kukana kwenu.
Unaweza kuhama kwenu moja kwa moja?
Naunga mkono hoja ya mjumbe wa kwanza kabisa!....mimi nalipa P.A.Y.E kila mwezi bila kutegea na sipo legelege katika kulipa hata kidogo!, sasa wahusika ulegelege wanautoa wapi?. Yaani nakataa kubebeshana mizigo iliyo/inayotokana na kukosa umakini kwa kundi fulani.
ReplyDeleteNjaa kali huleta wivu, na wivu unaua.
ReplyDeleteYAANI JAMANI PICHA KAMA ZA WAFUNGWA VILE.
ReplyDeletehii picha itakuwa kati ya mwaka 1997 na 1999, namuona Safiniel Mbaga maskini RIP dada, huyu wa kwanza ni Denis ALfred nadhani yuko BOT
ReplyDeleteRIP SAFINIEL, NILIKUWA NAE CLASS MOJA 1997-1999, nyambari nyangwine, peter kibatala, we riziwan,hassan mwemweta, kakere celestine, mtoroki majaliwa, irene kiwia, sundi fimbo and many more msikose!
ReplyDeletehi mtoa taarifa, basi fafanua zaidi ili watu wajipange c unajua time is money? muda ni saa ngapi? na kama wanachangiwa MUCE iweje walionza 2005 wasihusishwe ilhali ndio haswa watatueleza ugumu wa mazingira toka kiwe chuo kikuu kishiriki?