Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa OAU Dkt. Salim Ahmed Salim, huko Addis Ababa ambako viongozi hao walialikwa kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika. Ni nadra sana katika bara la Afrika na kwengineko duniani kuona Marais walioko madarakani na waliostaafu kuwa pamoja kwa amani na furaha namna hii. Tanzania Oye!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Tuombe Mwenyezi hali hiyo iendelee zaidi na zaidi.

    Licha ya baadhi ya wachache wasioitakia mema nchi yetu nzuri.

    Tanzania oyeeeeeeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Nchi zingine Maraisi Wastaafu kama hawapo Lupango wapo Uhamishoni!

    Hiyo ni balaa zaidi kwetu Afrika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2013

    Lingine Katiba ndio muhimu kuhakikisha hatuna Raisi Mstaafu atakayekuwa Gerezani ama kuishi nje ya Tanzania yetu.

    Tunataka tuwe na Katiba inayotetea zaidi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    Rais ajaye naye labda yupo hapo hapo kwa nyuma

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2013

    Kweli ni nadra sana ila kwa kweli Tanzania ni mfano wa kuiga kwa umoja na amani. Ila sisi sote tuna jukumu la kuilinda sana Amani yetu kwa kuwajibika kikamilifu katika majukumu yetu. Mungu ibaraki Tanzania. Natamani sana wimbo wa Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri uwe wimbo wa Taifa na ikibidi kuuboresha kuzingatia Amani na undugu wetu.
    My few cents.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2013

    Ni kitu kizuri kwa marais wote kuwa pamoja na kuishi kwa amani. Lakini pia tunataka huu ufisadi ukomeshwe, siyo kwamba tunaona tu wivu mtu akiiba bali pia ni kwa sababu kwa kuiba wanaibia wananchi wote, utakuta pesa zilizoibwa badala ya kujenga barabara ikasaidia watu wote, pesa inaibwa na mtu mmoja au kundi dogo la watu. Watanzania wa kawaida tunafanya kazi kwa bidii lakini inakatisha tamaa kuona mwingine anaiba pesa za nchi ambazo ni zetu watanzania wote kirahisi! Pili ni muhimu tukafuata demokrasia ya kweli kama nchi zingine hasa za kusini mwa africa, ningefurahi sana marais wetu wangekuwa wanashinda tuzo za MO zinazotolewa kwa wastaafu, inasikitisha sana kuwa hatuambulii kitu. Ninyi marais msiminye uhuru wa habari hata kama ni mbaya kiasi gani, tendeni haki.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2013

    that's good,Eeh Mola tujalie amani hii idumu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2013

    Wataacha kuwa na amani na raha wakati wote lao ni moja kutoka chama kimoja? Subiri Slaa ama Zitto wachukue nchi halafu utoe comment kama hiyo itamake sense maana nina uhakika kuna watakao kuwa Ukonga wakati mwaliko huu utakapo tolewa tena.

    ReplyDelete
  9. ChakubangaMay 28, 2013

    Sasa cha kujivunia hapo ni nini ? hakuna la zaidi hapo isipokuwa ni sera za kulindana, kuna ushahidi wa kutosha hapo viongozi waliopita (e.g Mkapa na ubinafsishaji wa mashirika) walifanya makosa na walitakiwa kuburuzwa mahakamani kujibu tuhuma zao lakini halijafanyika zaidi ya kulindana, kinachofuatia ni kila raisi amalizaye muda wake ana hakikisha anamsimika swahiba atakaye linda madhambi yake, je hilo ndilo tunalo jivunia ?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2013

    Kwa kweli ni jambo la furaha kwa kuwaona wakiwa pamoja wakati huu wa sherehe ya miaka 50 ya umoja wa afrika.jiulizeni viongozi wengine walitoka madaraka katika nchi zingine wapo wapi ? Tulinde amani na umoja wetu,tunaonewa wivu!kwa sisi tuliopita nchi nyingi duniani kuna tofauti sana na tunavyoishi hapa.kikubwa serikali ilikuwa madarakani ni kujenga nchi na kuinua hali ya maisha ya watu wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...