Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa OAU Dkt. Salim Ahmed Salim, huko Addis Ababa ambako viongozi hao walialikwa kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika. Ni nadra sana katika bara la Afrika na kwengineko duniani kuona Marais walioko madarakani na waliostaafu kuwa pamoja kwa amani na furaha namna hii. Tanzania Oye!
Home
Unlabelled
NANI KAMA TANZANIA?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tuombe Mwenyezi hali hiyo iendelee zaidi na zaidi.
ReplyDeleteLicha ya baadhi ya wachache wasioitakia mema nchi yetu nzuri.
Tanzania oyeeeeeeeeeee!!!!!!
Nchi zingine Maraisi Wastaafu kama hawapo Lupango wapo Uhamishoni!
ReplyDeleteHiyo ni balaa zaidi kwetu Afrika.
Lingine Katiba ndio muhimu kuhakikisha hatuna Raisi Mstaafu atakayekuwa Gerezani ama kuishi nje ya Tanzania yetu.
ReplyDeleteTunataka tuwe na Katiba inayotetea zaidi!
Rais ajaye naye labda yupo hapo hapo kwa nyuma
ReplyDeleteKweli ni nadra sana ila kwa kweli Tanzania ni mfano wa kuiga kwa umoja na amani. Ila sisi sote tuna jukumu la kuilinda sana Amani yetu kwa kuwajibika kikamilifu katika majukumu yetu. Mungu ibaraki Tanzania. Natamani sana wimbo wa Tazama Ramani Utaona Nchi Nzuri uwe wimbo wa Taifa na ikibidi kuuboresha kuzingatia Amani na undugu wetu.
ReplyDeleteMy few cents.
Ni kitu kizuri kwa marais wote kuwa pamoja na kuishi kwa amani. Lakini pia tunataka huu ufisadi ukomeshwe, siyo kwamba tunaona tu wivu mtu akiiba bali pia ni kwa sababu kwa kuiba wanaibia wananchi wote, utakuta pesa zilizoibwa badala ya kujenga barabara ikasaidia watu wote, pesa inaibwa na mtu mmoja au kundi dogo la watu. Watanzania wa kawaida tunafanya kazi kwa bidii lakini inakatisha tamaa kuona mwingine anaiba pesa za nchi ambazo ni zetu watanzania wote kirahisi! Pili ni muhimu tukafuata demokrasia ya kweli kama nchi zingine hasa za kusini mwa africa, ningefurahi sana marais wetu wangekuwa wanashinda tuzo za MO zinazotolewa kwa wastaafu, inasikitisha sana kuwa hatuambulii kitu. Ninyi marais msiminye uhuru wa habari hata kama ni mbaya kiasi gani, tendeni haki.
ReplyDeletethat's good,Eeh Mola tujalie amani hii idumu
ReplyDeleteWataacha kuwa na amani na raha wakati wote lao ni moja kutoka chama kimoja? Subiri Slaa ama Zitto wachukue nchi halafu utoe comment kama hiyo itamake sense maana nina uhakika kuna watakao kuwa Ukonga wakati mwaliko huu utakapo tolewa tena.
ReplyDeleteSasa cha kujivunia hapo ni nini ? hakuna la zaidi hapo isipokuwa ni sera za kulindana, kuna ushahidi wa kutosha hapo viongozi waliopita (e.g Mkapa na ubinafsishaji wa mashirika) walifanya makosa na walitakiwa kuburuzwa mahakamani kujibu tuhuma zao lakini halijafanyika zaidi ya kulindana, kinachofuatia ni kila raisi amalizaye muda wake ana hakikisha anamsimika swahiba atakaye linda madhambi yake, je hilo ndilo tunalo jivunia ?
ReplyDeleteKwa kweli ni jambo la furaha kwa kuwaona wakiwa pamoja wakati huu wa sherehe ya miaka 50 ya umoja wa afrika.jiulizeni viongozi wengine walitoka madaraka katika nchi zingine wapo wapi ? Tulinde amani na umoja wetu,tunaonewa wivu!kwa sisi tuliopita nchi nyingi duniani kuna tofauti sana na tunavyoishi hapa.kikubwa serikali ilikuwa madarakani ni kujenga nchi na kuinua hali ya maisha ya watu wako.
ReplyDelete