Salasala Vision Group (SVG), ni kikundi cha wakazi wa salasala Kilimahewa wapenda maendeleo kichoanzishwa mwaka 2012. SVG ilianzishwa ikiwa na malengo ya kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na ulinzi kwa maeneo ya Salasala Kilimahewa. 

Tangu SVG ilipoanzishwa mwaka jana, kundi hili limeweza kutekeleza mambo mengi katika mwaka mmoja; Kuanzisha ulinzi shirikishi katika maeneo ya Salasala kilimahewa, Kutengeneza uwanja wa michezo, kuchangia mavazi rasmi ya waendesha bodaboda, Kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wa SVG, Kuendeleza mahusiano na makundi mengine yenye malengo yanayoshabihiana na SVG.

 Katika kuazimisha mwaka mmoja, wanachama wa SVG wamepanda miti zaidi ya 1,500 katika maeneo yanayozunguka salasala kilimahewa. Zoezi hili endelevu linatarajiwa kuendelea mwezi wote wa Mei na kufikia zaidi ya miti 2,000 kupandwa.
Wana SVG wakijiandaa na zoezi la upandaji miti 1,500.
Wakazi wa kilimahewa wakichangamkia zoezi la kupanda miti.
Zoezi la upandaji miti liliendeshwa mitaa mbalimbali ya kilimahewa.
Watoto pia walishiriki kwenye zoezi la upandaji miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2013

    Kazi ni nzuri sana. Ila kina mama mbona hatuwaoni? Je wapo kwenye SVG pia? Au ni ya wanaume tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2013


    MVUA ZINAISHA NINYI NDIO MNAPANDA MITI!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2013

    Wakionyeshwa akina mama wengine wataanza kusema Ankal nisaidie nimpate yule; manake wanaume ni hatari sana. Wanawake ahueni wanaweza vumilia...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2013

    Good job wana SVG. We are happy to see that your group is aiming at restoring the glory of our wonderful City Dar es Salaam and its environs.


    Anonymous, Arusha

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2013

    Safiiii sana jaribuni kupanda miti itayopendezzesha mazingira ,Salasala itageuga Miami beach,

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2013

    Hongereni. Ila miti mmepanda karibu mno na barabara, hii ina adhari kwa maisha ya barabara na hatari kwa watumiaji wake.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2013

    Kwenye msafara wa mamba, kenge hawakosekani" msighazibike na baadhi ya comments. Mi naona ni good campain, mvua zijazo nitahamasisha mitaa ya kwetu. changes start with you.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...