Salasala Vision Group (SVG), ni kikundi cha wakazi wa salasala Kilimahewa wapenda maendeleo kichoanzishwa mwaka 2012. SVG ilianzishwa ikiwa na malengo ya kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na ulinzi kwa maeneo ya Salasala Kilimahewa.
Tangu SVG ilipoanzishwa mwaka jana, kundi hili limeweza kutekeleza mambo mengi katika mwaka mmoja; Kuanzisha ulinzi shirikishi katika maeneo ya Salasala kilimahewa, Kutengeneza uwanja wa michezo, kuchangia mavazi rasmi ya waendesha bodaboda, Kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wa SVG, Kuendeleza mahusiano na makundi mengine yenye malengo yanayoshabihiana na SVG.
Katika kuazimisha mwaka mmoja, wanachama wa SVG wamepanda miti zaidi ya 1,500 katika maeneo yanayozunguka salasala kilimahewa. Zoezi hili endelevu linatarajiwa kuendelea mwezi wote wa Mei na kufikia zaidi ya miti 2,000 kupandwa.
Wana SVG wakijiandaa na zoezi la upandaji miti 1,500.
Wakazi wa kilimahewa wakichangamkia zoezi la kupanda miti.
Zoezi la upandaji miti liliendeshwa mitaa mbalimbali ya kilimahewa.
Watoto pia walishiriki kwenye zoezi la upandaji miti.
Kazi ni nzuri sana. Ila kina mama mbona hatuwaoni? Je wapo kwenye SVG pia? Au ni ya wanaume tu?
ReplyDelete
ReplyDeleteMVUA ZINAISHA NINYI NDIO MNAPANDA MITI!
Wakionyeshwa akina mama wengine wataanza kusema Ankal nisaidie nimpate yule; manake wanaume ni hatari sana. Wanawake ahueni wanaweza vumilia...
ReplyDeleteGood job wana SVG. We are happy to see that your group is aiming at restoring the glory of our wonderful City Dar es Salaam and its environs.
ReplyDeleteAnonymous, Arusha
Safiiii sana jaribuni kupanda miti itayopendezzesha mazingira ,Salasala itageuga Miami beach,
ReplyDeleteHongereni. Ila miti mmepanda karibu mno na barabara, hii ina adhari kwa maisha ya barabara na hatari kwa watumiaji wake.
ReplyDeleteKwenye msafara wa mamba, kenge hawakosekani" msighazibike na baadhi ya comments. Mi naona ni good campain, mvua zijazo nitahamasisha mitaa ya kwetu. changes start with you.
ReplyDelete