Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa tangazo la nafasi za ajira ambalo limewekwa katika mtandao www.eastafricajobscarieer.com ni  batili. Mtandao huo ulichapisha tangazo hilo bila ridhaa ya Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hauna mkataba wowote wa kibiashara na mtandao huo.

Aidha, tangazo hilo ni nakala ya tangazo la ajira ambalo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulilitangaza katika magazeti ya Mwananchi, Nipashe, na Daily News tarehe 07, 10 na 14 Februari, 2012 na mchakato wa kujaza nafasi zilizotangazwa ulishakamilika.

Menejimenti ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya inawaomba radhi wote ambao wamepata usumbufu kutokana na tangazo hilo.

Limetolewa na:
 Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
S.L.P. 11360,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    Sawa, natumaini pia watachukuliwa hatua!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2013

    keshapewa mtu kwa mlango wa nyuma hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2013

    hayo matangazo ni ya mwaka jana (2012) isipokuwa yamejibadilisha kuwa (2013) kwa matatizo yao wa kiufundi. Kwa hiyo utakuta kuna matangazo ya application deadline December 2013!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...