Ujumbe wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) uko nchini Rwanda kubadilishana ujuzi na uzoefu na Rwanda kuhusu utekelezaji wa mradi wa kurahisisha na kuwezesha biashara (Trade Facilitation) kwa kutumia TEHAMA - Electronic Single Window System. Muda mfupi ujao TPA itaanza utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji, Forodha, wafanyaniashara na wadau wote wa Tanzania.
Ujumbe huo wa Tanzania unaongozwa na Mkuu wa mradi na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya TEHAMA-TPA Ndg. Phares Magesa wa kwanza kushoto, wengine ni Mathayo Ntandu, Jesse Shali na Kilian Chale ambao ni maofisa wakuu TPA.
Home
Unlabelled
UJUMBE WA TPA WATEMBELEA RWANDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kwa aibu kabisa tunakwenda kujifunza Rwanda na bado tunachekelea tu. Single Window System imeimbwa miaka mingapi leo hii ndio mnaenda kujifunza Rwanda?
ReplyDeletembona muonekano wa nchi za wenzetu ni safi sana na hata kama wana mji mdogo lakini muonekano wa kisasa na wenye unafasi na sio bongo yetu kujibana kwa kwenda mbele na machafu machafu kibao
ReplyDeleteHapo Rwanda kweli au Ulaya Ankal?? Haiwezekani iwe Rwanda. Hawa jamaa walikuwa kwenye vita kwa muda mrefu tu? Hivi Tanzania mbona haipo safi hivi?
ReplyDeleteenhee naratajia nyote mliochangia mwanzo ni Watanganyika sasa semeni wenyewe hii ni haki?
ReplyDeletechezea Phares magesa ww, this guy is very strutagic. town guy
ReplyDelete