Timu ya Tanzania ya kuogelea ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa kikombe cha mshindi wa Tatu jumla kwa kupata alama 230. 
Timu ya vijana kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wao wakiwa nyuma. 
Nahodha wa Timu ya Taifa ya kuogelea,Sonia Tumioto (katikati) akiwa na bendera ya Tanzania baada ya kupokea zawadi ya kikombe cha mshindi wa kwanza kwa wanawake.

Timu ya vijana ya kuogelea kutoka Tanzania imefanya vizuri katika mashindano yaliyoshirikisha timu 20 kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na mashindano hayo kufanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 May 2013 katika shule ya Aga Khan. Washiriki wa mashindano hayo walitoka katika nchi za Tanzania, Kenya, na Uganda ambazo kila mmoja alitaka kumshinda mwenzake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    Mashule ya walalahoi nayo wafundishwe kuogelea!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2013

    mdau hapo juu wataoge´lea kwenye madimbwi au visima hao walalahoi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2013

    Kwahi hamhaona kwa macho yenu hii "tripple heritage Watanzania" Sio watanzania hawa! Watanzania tunaogea mtoni tena tusubiri mvua zinyeshe maana mito nayo inakauka!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2013

    sura zao wengine wanafanana na watoto wa mabalozi nchini naona kuna wazungu na sura ambazo hazijakaa kibongo.Tujiandae kuunda timu iliyo na watanzania halisi, kesho hao mabalozi mda wao nchini ukiisha wanaondoka na watoto/vijana wao.

    ReplyDelete
  5. Michango yenu inafaa kwa maendeleo ya mchezo na watoto wetu. Kweli hapo juu kuna wazungu ambao siyo watanzania na kuna watoto wa kitanzania kama. Celina Itatilo, Reuben Monyo,Diya, na wengineo.Tunaomba leteni watoto wenu tuwafundishe atuwezi kufanikiwa bila wewe kuchukua hatua.

    Kyab'anyambala.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...