Timu ya Tanzania ya kuogelea ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa kikombe cha mshindi wa Tatu jumla kwa kupata alama 230.
Timu ya vijana kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wao wakiwa nyuma.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya kuogelea,Sonia Tumioto (katikati) akiwa na bendera ya Tanzania baada ya kupokea zawadi ya kikombe cha mshindi wa kwanza kwa wanawake.
Timu ya vijana ya kuogelea kutoka Tanzania imefanya vizuri katika mashindano yaliyoshirikisha timu 20 kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na mashindano hayo kufanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 May 2013 katika shule ya Aga Khan. Washiriki wa mashindano hayo walitoka katika nchi za Tanzania, Kenya, na Uganda ambazo kila mmoja alitaka kumshinda mwenzake.
Mashule ya walalahoi nayo wafundishwe kuogelea!!
ReplyDeletemdau hapo juu wataoge´lea kwenye madimbwi au visima hao walalahoi?
ReplyDeleteKwahi hamhaona kwa macho yenu hii "tripple heritage Watanzania" Sio watanzania hawa! Watanzania tunaogea mtoni tena tusubiri mvua zinyeshe maana mito nayo inakauka!
ReplyDeletesura zao wengine wanafanana na watoto wa mabalozi nchini naona kuna wazungu na sura ambazo hazijakaa kibongo.Tujiandae kuunda timu iliyo na watanzania halisi, kesho hao mabalozi mda wao nchini ukiisha wanaondoka na watoto/vijana wao.
ReplyDeleteMichango yenu inafaa kwa maendeleo ya mchezo na watoto wetu. Kweli hapo juu kuna wazungu ambao siyo watanzania na kuna watoto wa kitanzania kama. Celina Itatilo, Reuben Monyo,Diya, na wengineo.Tunaomba leteni watoto wenu tuwafundishe atuwezi kufanikiwa bila wewe kuchukua hatua.
ReplyDeleteKyab'anyambala.