Jamhuri ya Singapore (mji mkuu wake pia ni Singapore) ni nchi ya kisiwan Kusini Mashariki ya bara la Asia, ikiwa kusini mwa ncha ya Peninsula ya Malai na kilometer 137 kutoka mstari wa Equator. Ukubwa wa kisiwa kikuu cha Singapore ni km42 kwa urefu, wakati upana ni km23, na kina ukubwa wa kilomita za mraba 586.5. Ukubwa wake kwa jumla ukichanganya na visiwa vyake vyote ni kilomita za mrada 646.1(Zanzibar ina ukubwa wa kilomita za mraba 1464, ikiwa ni urefu wa km 86 na upana wa km36).
 Singapore ni nchi inayofanywa na visiwa 63, ikiwa imetenganishwa na nchi ya Malaysia na ghuba ya Johor kwa upande wa kaskazini na visiwa vya Riau vya Indonesia katika ghuba ya Singapore upande wa kusini. Ni nchi ya vikwangua anga ambayo imeanza mambo ya biashara miaka ya 1819, ambapo mwaka 1824 Waingereza waliitawala. Baada ya kukaliwa na Japan katika vita vya pili vya dunia nchi hii ndogo ilijipatia uhuru wake mwaka 1963, ambapo miaka miwili baadaye ikaja kujitenga na Malaysia waliyokuwa wakitawaliwa nayo kwa pamoja na Uingereza. 
Toka wakati huo imeendelea na kuwa moja ya nchi tajiri duniani, na ni mojawapo ya nchi nne zijulikanazo kama Chui wa Asia. Singapore ni nchi ya nne duniani kama kituo kikuu cha biashara, ambapo bandari yake ni moja kati ya tano ambazo zinafanya kazi sana duniani. Uchumi wake zaidi unategemea biashara ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi na bandari. 
Hivi sasa Singapore  ni ya tatu duniani kwa kuwa na watu wenye kipato kikubwa. Sifa zingine za nchi hii ni kuwa ya pili duniani kwa wingi wa ma Casino na kumbi za kuchezea kamari, ni mojawapo ya vituo vitatu vikubwa vya kuchujia mafuta na pia wanaongoza katika kufanya mategenezo ya meli. Benki ya dunia tayari imeitaja Singapore kama nchi iliyo nyepesi kufanya ama kufanyia biashara, na inaongoza kwa mambo ya biashara ya fedha za kigeni, ikiwa nyuma ya London, New York na Tokyo. 
Asilimia kubwa ya wakaazi wake ni Wachina, wkifuatiwa na watu wa mataifa ya Asia kama Wahindi, Malay na wengineo. Katika sense ya mwaka 2011, idadi ya watu wa Singapore ilikuwa milioni 5.18, ambapo milioni 3.25 ama asilimia 63 ni raia, na waliosalia (37%) ni wakaazi wa kudumu ama wafanyakazi wa mataifa mengine. Asilimia 23 ya raia wa Singapore walizaliwa nje ya nchi hiyo. Na hiyo huchanganyi na watu milioni 11 wanaotembelea kisiwa hicho kila mwaka. Lugha rasmi za Singapore ni nne. Kichina (49.9%) Kiingereza(32.3%) Ki-Malay (12.2%) na Tamil.
Kwa kuwa Singapore ni Kisiwa kidogo kinachokaliwa na watu wengi, idadi ya magari binfasi iko chini sana kwani uthibiti wake si mchezo ili kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa na foleni. Yaani mtu akitaka kununia gari binfasi inabidi alipe ushuru ambao ni mara moja na nusu ya bei ya hilo gari. Pia inabidi apate hati ya kukaa nalo hilo gari ya miaka 10, na bei ya kununulia hiyo hati ni sawa na bei ya gari aina ya Porsche huko Marekani! Yaani bei ya gari binfasi Singapore ni ya juu kuliko nchi yoyote inayoongea Kiingereza duniani. Hivyo ni mtu mmoja tu katika 10 mwenye gari binafsi. 
Cha kufurahisha ni kwamba kuna sheria kadhaa zinazodumisha nidhamu na usafi wa mazingira nchini Singapore. Ya kwanza ni kosa la jinai kutumia choo na kukiacha bila ku-flush. Ukikamatwa unapigwa faini hadi upate kizunguzungu. Ni kazi ya Askari polisi kuhakikisha vyoo vya umma viko safi kila mara. 
Sheria ingine kali ambayo ilitungwa toka mwaka 1968 ili kuhakikisha nchi inabaki safi ni hii ya usafi. Ni kosa la jinai kutupa taka ovyo barabarani. Faini yake ni dola 1,000 na pia unaweza ukaadhibiwa kutumikia adhabu ya kufanya kazi za kijamii. Ukitenda kosa hilo mara tatu unavalishwa alama inayosema “Mimi ni mchafuzi wa mazingira” 
Kula pipi ubani (Big G ama bazooka) nako kuna sheria zake, kwanza zimepigwa marufuku kuuzwa hovyo hovyo. Ukitaka unakwenda duka la madawa na unapoitafuna hakikisha masalia unayatupa kwenye pipa la taka. Ukikutwa umetema barabarani unapigwa bonge la faini. 
Mambo ya kukumbatiana na mpenzi wako hadharani pia ni marufuku. Hayo mambo kafanyieni ndani kwenu. Ukikutwa ni faini na hata kifungo jela. Haya ni baadhi tu ya maajabu ya Singapore ambako Ankal anakula vekesheni yake huku akiwa makini asibambwe kafanya kosa la aina hizo hapo juu.
 Sehemu ya jiji la Singapore linavyoonekana usiku
Ankal akiwa katikati ya jiji la Singapore usiku wa kuamkia leo
Ni saa moja na nusu asubuhi  ya leo Jumanne (Bongo ni saa 10 za Alfajiri) na Ankal analishangaa jiji la Singapore kabla ya kuweka ze fulanazzz pembeni na kuanza kula tizi la nguvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    Kaka Michuzi unaonekana huko mbali sana kimawazo au sijui unatafakari jambo gani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    eti eee! halafu anaonekana kazeeka ghafla! Ankal hukua hivi last two years! kulikoni swaiba wangu!

    ReplyDelete
  3. Ankal wewe umetembea na ahsante sana kwa taarifa kuhusu Singapore. Inabidi uandike kitabu cha kumbukumbu na picha nyingi za sehemu zote za dunia ulizotembelea. Picha ulizozikusanya ni nyingi mno na zinafaa kuwekewa kumbukumbu kama kitabu kimoja kikubwa sana cha picha na maelezo kwa vizazi vijavyo. Kiite 'Michuzi World Adventure'.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    Picha ya chini, Mshukuru mola umeshalamba chumvi kiasi cha kuotsha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    Kwa ulaji huo wa bata Jijini Singapuri kwa kweli Ankali kwa nini usirudi kuwa kijana kwa miaka 10 nyuma?

    Ohhh Michuzi mzee!, masema saana angalieni.

    Kwa uchanaji huo wa Bata atazeeka vipi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    Kwakweli yule Mdau wa Ugiriki aleyeomba mpango huu wa Vekesheni urudi amefanya jambo la maana.

    Maana Mjomba ametuchambulia kama Karanga jinsi Singapore ilivyo!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Uhhh Mji kama umeshushwa vile?

    Jamani na sisi tuuze gesi zetu na madini tuwe na miji kama hii.

    tunaomba Darisalama yetu na baadhi ya miji mingine TZ zionekane hivi baada ya miaka kadhaa mbele hapo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    Mji kuwa hivi ndio Wana harakati wa Gas Mtwara wanachopigania!!!

    Michuzi kwa nini usimweleze Mhe. Raisi Kikwete awashushie Mtwara iwe kama hiyo Singapore ili waache Maandamano yao wakalime na kuokota Korosho?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    Ankal mawazo lazima utakuwa nayo., usisahau kwenda kutembelea wizara ya urban planning, polisi na pia maktaba Kama ikiwezekana. Vinginevyo furahia vekesheni. Nilisahau. Angalia usiku ofisi za Serikali bila shaka na binafsi zinazimwa taa zote. Pia ulizia hiyo bandari mashuhuri ina wafanyakazi wangapi? Ehe, na uelewa wa wananchi aw kawaida juu ya nchi yao. Tujuze. All the best.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2013

    Kila kitu kinawezekana iwapo uadilifu na nidhamu ya matumizi itazingatiwa. Singapore wala hawana natural resources nyingi kama nchi zetu, lakini wamejipanga kutumia nafasi yao ya kijiografia kwa maslahi ya jamii yao.

    Shame to African leaders.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2013

    Ankal usiache kutembelea Marina Bay na Flower dome, uwaelezee wadau jinsi hawa wenzetu wasiokua na mali asili kama zetu ila ni moja ya nchi zinazoongoza kwa utalii duniani

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2013

    Hii ndio ze fulanazzz?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2013

    You have made my day...Fulanaz oooye.
    Misupu this is not stori,ni jambo lakumtia mbantu aibu kubwa sana.Mtu akisoma mafanikio ya ndugu zetu hao ni lazima ajiulize, what is wrong with me, what is wrong with my fellow Africans, why are we still eating dust. Sifikiri umesahau kutaja mashimo ya alimasi au dhahabu au mafuta au gesi huko uliko, ukweli ni kuwa hawana, lakini mimi kwetu tele.Bado tu nala vumbi na matope. I will look in the mirror again and ask the man I see for answers.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2013

    Ankal vipi tena wangu, mbona umezeeka ghafla hivo nani anasababisha hii.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2013

    Ankali fanya upite na hapa Malaysia uchukue taswira kidogo ila Singapore si mchezo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 04, 2013

    Ankal usibebe unga tu, watakukata kichwa hawa jamaa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2013

    Usiangalie sura tu, angalia umri na majukumu! Inawezekana na shughuli kubwa ya kutujuza mambo bado anaonekana kijana

    sesophy

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 04, 2013

    ankali kila siku unatuwekea vikwangua anga vya kibongo ambavyo haviishi kuanguka vyenyewe sasa je umeona vikwangua anga vya kikweli?

    ankali unafikiria ujenzi wa vikwangua anga vya nchi yetu ambavyo havina mpangilio hivi tutaweza kuwa na vikwangua anga vyenye mvuto kama hivyo?

    ule ujenzi wa dasalame ni ujenzi wa kiholela na ujenzi mchafu sana serikali husika ya mambo ya ujenzi wa majumba ipo nyuma miaka 100

    mtu wowote akiwa na kiwanja chake katikati ya jiji atajenga jinsi anavyotaka yeye

    wenzetu wanasheria ya ujenzi wa katikati ya jiji ukitaka kujenga ni lazima upeleke ramani ya mjengo wako wakiona haufanani na eneo hilo hupewi kibali cha kujenga

    wahusika wa ujenzi wa majumba hutoa ramani ya mijengo inayotakiwa kujengwa baadhi ya maeneo ya jiji ili kupendezesha jiji na sio ujenzi wa kiholela

    jambo la mwisho namalizia ankali chonde chonde tafuta muda wa mapunziko kwani afya ni muhimu kwa maisha yako unaonekana week sana uzee unakuja kwa kasi sana naona kutokana na kupoteza rafiki zako wengi kwa kipindi kifupi pole sana.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 04, 2013

    Handsome man Michuzi hamumuoni?

    Ankali handsome man kabisa wakati wapo Mababu wenye namba ndefu mno kama 80+ na wangali wanatesa tu wanakaba hadi Penati!

    Hao wanaosema Michuzi kazeeka wamechemsha, hivi mwanaume anazeekaga?

    Hebu angalia Mzee wa Miaka 75 anao uwezo wa kuchukua Mabinti wabichi kabisa ili mradi Jogoo lake linawika na mfuko wake upo njema!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 04, 2013

    Ankali hao wanaodai umezeeka hebu pitia Malaysia anakodai Mdau wa 15 ili angalau ufanye scrub na facial kidogo utoe makunyanzi!

    Lakini wasije lalamika tena, ohhh Ankali amerudi kijana atatupindulia watu wetu!, ohhh, ohhh, ohhh maana Vijana hawachoki malalamiko kama Mama ntilie anavyodaiwa aongeze mchuzi kwenye ubwabwa, akiongeza ohhh mchuzi umeweka mwingi!

    Maana Ankali 'ukubwa' unakujia kipindi ambacho ni Alfajiri na ndio nyota inachomoza!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 04, 2013

    JAMANI HUYU SIYO ANKALI,HUYU BABA YAKE JAMANI NA MICHUZI.MZEE KABISAAA BWANA.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2013

    Fungua: http://www.kwanzajamii.com/?p=3206
    usome makala ya born Again pagan kuhusu kujikwamua kwa Singapore!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 04, 2013

    Dah watu muna mawazo potofu sana, yaani munataka majumba makubwa ili iweje ? Wakati ukiamka unafikiria utakula nini au utalala wapi mana mvua ikinyesha hapo kibarazani kwa watu utaroa si ndo godoro lako ?

    Ukisikia nchi fulani ina maendeleo na tajiri, ujue wananchi wake wanalala ndani tena nyumba standard,wanapata lishe, huduma za afya,elimu bure, tena wakati wowote unapotaka kusoma, haichagui umri au ulimbia shule.

    Sasa Tz kama kweli tunataka maendeleo, NSSF ichukue fedha kutoka kwa rasilimali zetu watujengee makazi , vituo vya afya ambavyo vitavyo kidhi mahitaji yetu, elimu iboroeshwe na bure. Majumba marefu yatakuja wenyewe.

    Think think, si unamuona ankle hapo anavyofikiri ? waamshee

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2013

    Tabasamu kidogo Ankal.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 05, 2013

    Huki siyo kuzeeka, ni dalili ya kuwa overworked, geee anaonekana kama yuko 70+

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...