Taifa Stars imetua Marrakech, Morocco, salama salimini tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia ilikaa timu ya Ivory Coast ilipokuja kucheza na Morocco. Kikosi hicho kina wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili leo Juni 4, 2013 mwaka huu saa 8 mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambapo timu yao ya TP Mazembe ilikuwa na mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ambapo nyumbani Tanzania itakuwa ni saa 5 usiku.
Kila la kheri Stars.Tucheze mchezo huu kwa Malengo na Hesabu "Za kufa mtu" huku OBJECTIVE kubwa ikiwa ni kupata ushindi.Ni bahati nzuri kwetu kwamba Mechi ya Gambia na Ivory coast itaisha mapema kabla ya huu mchezo wetu na Morocco(Msimamo wa kundi letu utakuwa umefahamika mapema!).Kwa mujibu wa Tovuti ya FIFA mchezo wa Gambia na Ivory coast utaanza saa 1.30 jioni saa za Afrika Mashariki.Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDeleteDavid V
taifa stars timu piga bao 3 za fastafasta hao morroco ili wachangikiwe mapema
ReplyDeletekumbuka biashara asubuhi jioni mahesabu tunataka kuwaona kwenye luninga mkikipiga brazil na the netherlands