Wakaazi wa jiji la dar es Salaam wameendelea kuchangamkia matumizi ya huduma ya M pesa kwa kufanya malipo ya bidhaa mbalimabli huku wakitoa wito kwa watanzania wengine kuendelea kupokea na kutumia mapinduzi hayo makubwa ya kiteknolojia katika sekta ya simu. Hayo yamebainishwa na wakazi wa Dar es Salaam wakati Vodacom ilipoendesha zoezi la uhamashishaji wa wateja kutumia huduma ya Mpesa kulipia manunuzi ya bidhaa wanayoyafanya katika maduka ya shoppes ya jijini Dar es Salaam. 
 Happy Lema, Moja ya wateja walionunua bidhaa na kufanya malipo ya kupitia hudum ya M pesa amesema kuwa huduma hiyo imerahisisha maisha kwao kwa kuwawezesha kufanya malipo kwa njia ambayo ni rahisi na salama zaidi na wakati wowote.
 “Sasa huduma ya M pesa ni zaidi ya kutuma na kupokea fedha, imetuwezesha watanzania kupata huduma mbalimbali kwa wakati wote na kuwa na fedha wakati wote hivyo kuwa na uhakika wa kupata huduma yoyote mtu anayohitaji, alisema Happy na Kuongeza kuwa. “Kukua huku kwa matumizi ya huduma hii ya M PESA ni maendeleo makubwa ya kiteknolojia hivyo ni vyema watanzania wakatumia huduma hii kwani, bado kuna watu wana utamaduni wa kubeba pesa nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hata kuhatarisha usalama wao lakini mtu anaweza kuwa kwenye usalama zaidi akitumia huduma ya M - pesa,” 
 Happy alisema ni vyema sasa watanzania wakaacha kufanya mambo kwa mazoea kwa kubeba fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine utaratibu ambao sasa umepitwa na wakati. “Kumelipotiwa kuwepo kwa matukio kadhaa ya watu kuvamiwa na kuporwa fedha wakiwa njiani kwenda benki au wanapoenda kufanya manunuzi, ni vyema sasa tukaachana na utamaduni huu hatarishi, sasa mtu unaweza kuweka feha katika akaunti yako ya M pesa na kuzihamishia katika benki kwa urahisi na usalama zaidi. 
 Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim amesema kuwa Vodacom imeendelea kuiimarisha huduma ya M pesa pamoja na kuiongezea wigo wa matumizi kwa kuyaweka pamoja makampuni mbalimbali ya bidhaa na huduma hapa nchi. “kwa kutumia huduma yetu ya Mpesa tunawahakikishia watanzania kuwa zaidi ya kutuma na kupokea fedha, kufanya manunuzi katika sehemu mbalimbali, kulipia ada za shule na vyuo, matibabu na huduma nyingine za kijamii kama huduma za maji na umeme
"Bado Vodacom tumeendelea kuhakikisha kupitia huduma yetu ya M pesa tunaondoa kabisa utamaduni wa watu kubeba fedha kutoka sehemu moja kwenda nyingine,” alisema Mwalim na kuongezea kuwa kupitia huduma ya Mpesa sasa mteja anaweza kufanya malipo na kulipia manunuzi kwa kampuni zaidi ya 250 nchini
Mteja wa Vodacom M Pesa, Happy Lema akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana mara baada ya kulipia bidhaa kupitia huduma ya M pesa, Dar es Salaam, jana sasa wateja wa kampuni ya Vodacom wanaweza kulipia bidhaa zao kwa njia ya M pesa katika maduka ya Shoppers. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje, Salum Mwalimu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Salum Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari katika mara baada ya zoezi la kuwahamasisha wateja wa mtandao huo kununua na kufanya malipo ya bidhaa kupitia huduma ya M pesa katika maduka ya Shoppers jijini Dar 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...