Unapozungumzia mchezo wa ngumi au ndondi nchini ujerumani Jina la Bondia wa kike mwafrika Bintou Yawa Schmill a.k.a "The Voice" ndiye anayemudu uringo "Boxing Ring" na kulipeperusha bara la Afrika ughaibuni. 
Bondia huyo kike Bintou Yawa Schmill mwenye maskani kule Drackenburg nje kidogo ya mji wa Bremen,amekuwa kivutio kwa washabiki wa kimataifa na tishio kwa wapinzani wake anapokuwapo ulingoni. 
Boxer Bintou Yawa Schmill mzaliwa wa Togo mwenye makao yake nchini ujerumani alianza kucheza ngumi akiwa na umri mdogo na kushinda mara 14 katika mashindano 24 na mara 4 K.O ,katoka draw mara 2 uzito wa Walterweight 63.5 Kg, katika ngumi za ridhaa. 
 Kuanzia mwaka 2007 Boxer Bintou Yawa Schmill a.k.a "The Voice" aliamua kucheza kungumi za kulipwa  na tyari amepigana na kushinda professional Record 4 na Ushindi wa K.O mara 3. Boxer Bintou Schmill kwa sasa kajiandaa kupambambana na bondia yeyote yule wa kike na mahala popote duniani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2013

    Ankal naomba namba ya huyu demu. Nataka nianzishe uchumba.Samahani natanian tu asije akaanifanya gunia la mazoezi, lishe wenye ugali tembele.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2013

    Anony wa No.1
    Anasema alikuwa anatania tu ! utani wenyewe unaonyesha jinsi gani ? fikira za baadhi ya wengi wetu tulivyo jawa na upimbi upimbi ulichanganyika na wingi wa mawazo finyu,baadala ya kufikiria nasi dada zetu tutawafikisha vipi kiwango cha juu kimichezo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...