Na Bazil Makungu Ludewa

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda jela miezi kumi na mbili na kunywang’anywa leseni ya udereva na kisha kufungiwa kutoendesha gari lolote katika maisha yake Edward Mliwa kwa kusababisha majeraha kwa watu watano baada ya kupata ajali kwa uzembe. 

 Akisoma hukumu hiyo iliyochukua takribani masaa mawili hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna alisema kuwa mahakama yake imeridhika na ushahidi ulioletwa mbele yake na upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi kumi na mbili jela au kulipa faini ya sh hamsini elfu (50,000) kwa kila kosa.

Lukuna mshtakiwa Edward Mliwa anashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo kuendesha chombo cha moto kwenye barabara ya umma kwa uzembe na kusababisha ajali iliyowajeruhi watu watano kinyume na sheria chini ya kifungu 41, 50 na 63(2) cha sheria barabarani sura ya 168.

Hakimu mkazi mfawidhi akaendelea kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 12 mwaka 2012 katika kijiji cha Masasi barabara ya Ludewa Manda wilayani Ludewa ambapo alikuwa akiendesha gari aina ya center yenye namba za usajiri T 715 AZU akiwa amebeba abiria kupita kiasi.

Awali mshtakiwa alikiri kosa moja tu ambalo ni kusababisha majeraha kwa abiria watano lakini akakana kuhusika na kosa na uzembe akiwa na chombo cha moto hata hivyo mahakama hiyo imeiamuru mamlaka ya mapato nchini TRA kuifungia leseni ya mshtakiwa maisha kutokana na makosa hayo.

Akiomboleza mahakani hapo Edward Mliwa akaiomba mahakama kumwonea huruma na kumpunguzia adhabu kwa sababu anayofamilia inayomtegemea, hata hivyo alilipa faini na kupona kwenda jela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    Inatisha hii adhabu
    Nafikiri angeua mtu, angehukumiwa kukatwa kichwa kwa shoka butu.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    Hizi adhabu ndo zinatakiwa. Ajali zitokanazo na uzembe zingekuwa ndoto Tanganyika!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    Scapegoat!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2013

    Mafisadi ya EPA nayo tuyapeleke kwa Hakimu huyu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2013

    Jamani mbona ni wengi tu kwa Tz wanaostahili hizo adhabu ila hawapati adhabu hata kidogo. Huyo namhurumia sana mana inakuwa kama kumuonewa ukilinganisha na wengi wanaoachiwa na hata kusababisha vifo vya watu wengi tu. Kama mmeanza iwe hivyo kwa kila dereva anayekosea!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2013

    Nawahakikishieni kama atakaa jela hiyo mienzi mniite humbwa! Watahonga tu kama wafanyavyo wengine na atatoka! Ingekuwa hii ndio sheria consistently kweli lakini hapa! Nguvu ya sida tu labda masikini awe hana hongo lakini atatoka tu.

    ReplyDelete
  7. Ankal shikamoo. Naomba tafadhali unirushie hili ombi langu hewani. Ingawaje watu wataliponda lakini mwisho wa siku nitapata ufumbuzi. Mimi ni msichana wa kitanzania na nina miaka 26 sasa. Nipo Uingereza kimasomo kwani nachukua masters katika mji uliopo nje kidogo ya London.
    Shida yangu kubwa ni kwamba natafuta marafiki wa kitanzania waliopo hapa Uingereza maana kwa kweli ankali nchi za watu zinachosha sana especial pale ambapo hauna mtu wa kubadilishana naye mawazo. Kwamaana tokea nimefika hapa mwanzoni mwa mwaka huu mpaka leo sijawahi kusikia au kuongea kiswahili hata kidogo, na chuoni waafrika wengi ni kutoka West, South na Central Africa. Basi hapo ni tabu tupu..!
    Please Ankal naomba husiache kunirushia hewani hii post yangu. Napatikana katika email yangu swailaura@yahoo.co.uk Ahsante Ankal nashukuru sana na ninaamini nitapata marafiki wa kubadilishana nao mawazo. Napenda kukutakia weekend njema.
    Laura Swai,
    Uingereza

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2013

    Ameonewa huyo kutokana na ajali nyingi zinazotokea lakini mamlaka zinazohusika hazichukui hatua na pengine kama hukunmu zingetolewa kama hizi kwa waliomtangulia asingefanya hili kosa, otherwise hakimu amefanya kazi yake vizuri though isiinyie kwa huyu tu ili kuonyesha fairness kwa wengine

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2013

    Mie naona huyu dreva akate rufaa.
    Nionavyo mimi ameadhibiwa kupita kiasi, au wanavyosema wajuzi
    Punishment should be proportionate to the gravity of the crime.
    Ilivyoripotiwa ni kwamba alikuwa mzembe, ok,hakuua mtu bali ALIJERUHI watu watano, sio mia tano.Basi angalia adhabu yake
    1.Kunyang'anywa liseni ya udereva
    2.Faini shilling hamsin elf 50,000
    3.Jela miezi kumi na mbili, yaani mwaka mzima
    $.Kisha kufungiwa kuendesha gari lo lote katika maisha yake
    Audhubillah
    Huu ni ukatili, jamaa akitoka jela, kama yeye ni professional driver, ajifunze ufundi mpya,wizi?
    Kama kuna wakili msamaria, hala hala msaidieni huyu binAdam.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2013

    Hivi hawa mahakimu huwa wanahukumu kwa kufuata vitabu tofauti au???maana hukumu zingine duu kiboko, japo huwa twalalama tukitaka hawa madereva wazembe wenye kusababisha ajari wahukumiwe ila hukumu hii nadhani ni chachu ya zingine zijazo.....hahhahaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...