Na Bazil Makungu Ludewa
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda
jela miezi kumi na mbili na kunywang’anywa leseni ya udereva na kisha
kufungiwa kutoendesha gari lolote katika maisha yake Edward Mliwa kwa
kusababisha majeraha kwa watu watano baada ya kupata ajali kwa uzembe.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua takribani masaa mawili hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna alisema kuwa
mahakama yake imeridhika na ushahidi ulioletwa mbele yake na upande
wa mashtaka na kwamba mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi kumi na
mbili jela au kulipa faini ya sh hamsini elfu (50,000) kwa kila kosa.
Lukuna mshtakiwa Edward Mliwa anashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo
kuendesha chombo cha moto kwenye barabara ya umma kwa uzembe na
kusababisha ajali iliyowajeruhi watu watano kinyume na sheria chini ya
kifungu 41, 50 na 63(2) cha sheria barabarani sura ya 168.
Hakimu mkazi mfawidhi akaendelea kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo
Novemba 12 mwaka 2012 katika kijiji cha Masasi barabara ya Ludewa
Manda wilayani Ludewa ambapo alikuwa akiendesha gari aina ya center
yenye namba za usajiri T 715 AZU akiwa amebeba abiria kupita kiasi.
Awali mshtakiwa alikiri kosa moja tu ambalo ni kusababisha majeraha
kwa abiria watano lakini akakana kuhusika na kosa na uzembe akiwa na
chombo cha moto hata hivyo mahakama hiyo imeiamuru mamlaka ya mapato
nchini TRA kuifungia leseni ya mshtakiwa maisha kutokana na makosa
hayo.
Akiomboleza mahakani hapo Edward Mliwa akaiomba mahakama kumwonea
huruma na kumpunguzia adhabu kwa sababu anayofamilia inayomtegemea,
hata hivyo alilipa faini na kupona kwenda jela.
Inatisha hii adhabu
ReplyDeleteNafikiri angeua mtu, angehukumiwa kukatwa kichwa kwa shoka butu.
Ibrahim
Hizi adhabu ndo zinatakiwa. Ajali zitokanazo na uzembe zingekuwa ndoto Tanganyika!
ReplyDeleteScapegoat!
ReplyDeleteMafisadi ya EPA nayo tuyapeleke kwa Hakimu huyu!
ReplyDeleteJamani mbona ni wengi tu kwa Tz wanaostahili hizo adhabu ila hawapati adhabu hata kidogo. Huyo namhurumia sana mana inakuwa kama kumuonewa ukilinganisha na wengi wanaoachiwa na hata kusababisha vifo vya watu wengi tu. Kama mmeanza iwe hivyo kwa kila dereva anayekosea!
ReplyDeleteNawahakikishieni kama atakaa jela hiyo mienzi mniite humbwa! Watahonga tu kama wafanyavyo wengine na atatoka! Ingekuwa hii ndio sheria consistently kweli lakini hapa! Nguvu ya sida tu labda masikini awe hana hongo lakini atatoka tu.
ReplyDeleteAnkal shikamoo. Naomba tafadhali unirushie hili ombi langu hewani. Ingawaje watu wataliponda lakini mwisho wa siku nitapata ufumbuzi. Mimi ni msichana wa kitanzania na nina miaka 26 sasa. Nipo Uingereza kimasomo kwani nachukua masters katika mji uliopo nje kidogo ya London.
ReplyDeleteShida yangu kubwa ni kwamba natafuta marafiki wa kitanzania waliopo hapa Uingereza maana kwa kweli ankali nchi za watu zinachosha sana especial pale ambapo hauna mtu wa kubadilishana naye mawazo. Kwamaana tokea nimefika hapa mwanzoni mwa mwaka huu mpaka leo sijawahi kusikia au kuongea kiswahili hata kidogo, na chuoni waafrika wengi ni kutoka West, South na Central Africa. Basi hapo ni tabu tupu..!
Please Ankal naomba husiache kunirushia hewani hii post yangu. Napatikana katika email yangu swailaura@yahoo.co.uk Ahsante Ankal nashukuru sana na ninaamini nitapata marafiki wa kubadilishana nao mawazo. Napenda kukutakia weekend njema.
Laura Swai,
Uingereza
Ameonewa huyo kutokana na ajali nyingi zinazotokea lakini mamlaka zinazohusika hazichukui hatua na pengine kama hukunmu zingetolewa kama hizi kwa waliomtangulia asingefanya hili kosa, otherwise hakimu amefanya kazi yake vizuri though isiinyie kwa huyu tu ili kuonyesha fairness kwa wengine
ReplyDeleteMie naona huyu dreva akate rufaa.
ReplyDeleteNionavyo mimi ameadhibiwa kupita kiasi, au wanavyosema wajuzi
Punishment should be proportionate to the gravity of the crime.
Ilivyoripotiwa ni kwamba alikuwa mzembe, ok,hakuua mtu bali ALIJERUHI watu watano, sio mia tano.Basi angalia adhabu yake
1.Kunyang'anywa liseni ya udereva
2.Faini shilling hamsin elf 50,000
3.Jela miezi kumi na mbili, yaani mwaka mzima
$.Kisha kufungiwa kuendesha gari lo lote katika maisha yake
Audhubillah
Huu ni ukatili, jamaa akitoka jela, kama yeye ni professional driver, ajifunze ufundi mpya,wizi?
Kama kuna wakili msamaria, hala hala msaidieni huyu binAdam.
Ibrahim
Hivi hawa mahakimu huwa wanahukumu kwa kufuata vitabu tofauti au???maana hukumu zingine duu kiboko, japo huwa twalalama tukitaka hawa madereva wazembe wenye kusababisha ajari wahukumiwe ila hukumu hii nadhani ni chachu ya zingine zijazo.....hahhahaha
ReplyDelete