Na Vicky Kimaro, Mwananchi

Dar es Salaam. “Madaktari waliponiambia kuwa watoto wangu wameungana nilichanganyikiwa, niliona dunia imenigeuka, sikuwahi kuwaza nitakutana na kitu cha namna hii katika maisha yangu.”
Ni maneno ya binti kutoka kabila la Wandali ambalo asili yake ni Mbeya, Grace Joel (19), ambaye Februari 20 mwaka huu, alijifungua mapacha wa kiume ambao wameungana katika sehemu ya kiunoni.
Mwanadada huyo anasema hakuamini macho yake pale madaktari wa Hospitali ya Uyole iliyopo mkoani humo walipomwambia kuwa watoto wake wameungana na hivyo kupewa rufaa ya kwenda kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa wa Mbeya.
"Wakati wa ujauzito wangu sikuwahi hata siku moja kuhisi kuwa ningeweza kuzaa watoto wakiwa kwenye tatizo hili, sikuwahi kuumwa zaidi ya kuvimba miguu tu na  hiyo ni hali ya kawaida kwa mjamzito yeyote." anasema Grace ambaye kwa sasa anahitaji msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha ya watoto wake.
Licha ya umri huo mdogo, amejikuta kwenye hali ya mateso na uchungu mwingi baada ya familia yake, hususani mume wake, Erick Mwakyusa kumtelekeza kwa kile alichodai kuwa hana haja na watoto walioungana.

Kwa msaada ili kuokoa maisha ya 
watoto hawa piga namba 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2013

    watoto wazuri mno!tunawaombea mafanikio ya upasuaji na pia wawe baraka katika maisha ya mama yao ambaye ameumizwa kwa namna nyingi.God bless

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2013

    "..Utakalo lifanyike duniani na kama mbinguni..." Kazi ya Mungu haina makosa,Maanani awajalie upasuaji uende slama salimini- Amen.

    ReplyDelete
  3. ChakubangaJune 22, 2013

    Why why why wananchi ndio wachangie serikali iko wapi ? Kama serikali inaweza kugharamia matibabu ya wabunge na mawaziri nje ya nchi ambao wanajiweza kipesa na mara katika case ambazo zingeweza kutibiwa nchini, Why not paying for these poor children in needs.
    Na raisi anakwenda nje badala ya kuomba vifaa vya mahospitali anaomba football academy !

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2013

    Conjoined twins, well i wish procedure like this and all of its kinds could be done right here in Tanzania. I don't know when we gonna stop this mentality of sending out even a simple procedure.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2013

    siku wakitokea hao madaktari wa India waamue kufungua hospital hapa Tanzania watakusanya pesa nyingi sana, maana kuacha hii issue ya watoto walio ungana ambayo ni serious, kuna issues unakuta mbunge kalalia mkono usiku sasa kaamka unauma kidogo anakimbilia India, kuna yule aliye ng'atwa na nyuki akakimbizwa India kwa matibabu zaidi, na yule mke wa Fulani aliye kimbizwa India sababu koo lake lilikuwa lina muwasha. Haya nawatakia watoto hao upasuaji mwema kabisa.

    ReplyDelete
  6. Ni maombi yangu kuwa Mungu afanikishe operesheni hii.AMEN

    ReplyDelete
  7. mama luqmanJune 23, 2013

    pole sasa mama mungu atakujalia watatenganishwa wanao usikate tamaa amini mungu ni mwema na ana uwezo wake wa kipekee kabisa amin.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2013

    UTUKUFU UNA YEYE MILELE HATA MILELE-AAMINA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2013

    Why,why,why
    I can understand the frustrations za mwananchi.This is terrible, but the government can not do all that there is to be done.Kwa upande wa matibabu nakubali kuwa matatizo yangepewa priority, but we have to share the little we have.Medical care is very very expensive and with modern advances its sky-high.Did you know if the government sent ten people abroad for a super-duper subcutaneous implantable cardioverter-defibrillator, that would cause a massive blackhole in the ministry of health budget.There would be little left to treat kids with malaria in Mwananyamala Kuna mabilionea wabongo, jee mpo wapi ndugu zangu, msaidieni huyu mtoto.
    Ibrahim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...