JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
 

               SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA
BW. ALBERT MANGWEHA, (Man Ngwair)
1/06/2013.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika  Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne  tarehe 28 Mei, 2013. 
Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi. 
Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki  kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini. 

Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote  na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba. 
Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa  yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala pema peponi.”
  

Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2013

    Yaani hakuna mtu ku edit hii habari? Jina mmetumia "Mangweha" mara Mangwea tujue jina lipi lake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...