Habari yako mkuu wa Libeneke.

Mimi naomba msaada wako maana kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikipata unsolicited emails kutoka kwa watu wanajiita Dar-Insight ambao wanatuma matangazo ya ajabu ajabu ambayo mi hayanihusu, siyataki na yananijazia tu inbox yangu. Ubaya ni kwamba email zao hazina hata option ya ku-unsubscribe. Nimewaandikia mara kadhaa kuniondoa kwenye mailing list yao bila mafanikio kwani bado naendelea kupata email zao kadhaa kila siku.

Sasa naomba msaada kwa wadau kwanza kujua inakuwaje hawa watu wa push tu matangazo yao kwa watu ambao hawakujuandikisha wala kukubali kutumiwa matangazo yao. Sijui hata email yangu waliipata wapi.

Pili naomba kujua kwamba kwa sheria za Tanzania, ni hatua gani naweza kuchukua kuwashughulikia hawa jamaa maana email zao binafso zinanikera sana na nimejaribu njia ya kiungwana ya kuwaandikia email kuwaomba wasinitumie wamegoma kufanya hivyo. So hatua gani naweza kuchukua?

Asante sana, siku njema na sikukuu njema ya kupaa kwa Mtume.

Mdau anayekerwa na Dar-Insight.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    Nashukuru mdau wa hapo juu kuleta hii hoja au malalamiko hapa. Mie pia Napata hizo e-mails kama ulivyoandika na sijawahi kuwapa e-mail address yangu wala sizihitaji na hazina msaada wowote kwangu ila ndio kila kukicha wanatuma tu. Mie pia mniondoe kwenye watumiwaji hizo e-mails. Labda Michuzi anaweza kutusaidia kuwa-contact na kuwafahamisha haya malalamiko kwa kuwa yeye ni mtu wa blog nauhakika watamsikiliza. Hawa watu kweli mdau kama ulivyosema wanatakiwa kushtakiwa kabisa. Wahusika kama mnasoma hapa jirekebisheni haraka iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    hawa jamaa na wengine wa staili hizo ni kero sana..
    Jaribu kuwaspam ama block kabisa hiyo adress yao
    Unaweza kublock ile domain yao kwa ujumla.. il kama wanatumia email za public kama Gmail au yahoo inaweza kuwa ngumu kublock domain nzima

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2013

    Bora mmesema

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2013

    Mimi naona imefika wakati sasa Tanzania wakaweka sharia ambayo itamlinda consumer kwa media act. Mimi nilipata tabu kwa auto sms kutoka Zantel! kero zaidi hazina mudamaalum hata usiku wamanane zinakuja advertising msg.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2013

    Naona ndio umejua kutumia e mail hivi karibuni! Unachotakiwa kufanya ni ku 'MARK AS SPAM' Yahoo wana option ys 'REPORT SPAM' kwenye e mail yako. Haya matangazo hako mengi sana duniani na hii ndo njia ya kuyashughulikia

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2013

    Wengine wanajiita ZOOM MAIL SHOTS nao wanatabia ya kutuma emails za matangazo imefika wkt wa kuomba turidhie matangazo yao. BINAFSI NAKERWA NA ZOOM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...