Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana walifanya ziara katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo kwa lengo la kutembelea ofisi hizo na kuangalia mazingira ya kazi. 

 Wajumbe walioteuliwa hivi karibuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo, Mwanaidi Mtanda, Ezekiah Oluoch, Donan Mmbando, Mohamed Mohamed, Lydia Choma, Mohamed Hashim, Charles Kajege na Emanuel Humba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto walipozuru Makao Makuu jana.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Eugen Mikongoti akitoa maelezo ya namna ya kuhifadhi kumbukumbu za wanachama katika kituo cha kisasa cha Mfuko huo.
Wajumbe hao wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa NHIF namna ya upatikanaji wa haraka wa kumbukumbu za wanachama zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Wajumbe wakiendelea kujifunza zaidi katika kituo cha kuhifadhia kumbukumbu.
Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba (wa nne kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...