Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa Bendi ya The Kilimanjaro (wana njenje),Waziri Ally pamoja na Mwana FA baada ya kukabidhi tuzo ya heshima kwa bendi hiyo,wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanamuziki mbali mbali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Muziki wa Kizazi,Kala Jeremiar akitoa shukrani zake kwa mashabiki waliompigia kura na kumuwezesha kupata Tuzo tatu zikiwa ni Msanii Bora wa Hip Hop,Mtunzi Bora wa Mashairi ya Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop kwa kipindi chote cha Mwaka 2012/13.Kulia ni Msanii Shilole aliepanja jukwaani Kumsindikiza.Hafla hii ya utoaji tuzo imefanyika Usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop hapa nchini ambaye sasa amepotea kidogo kwenye Gemu hilo,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crezy G.K akiwasalimia mashabiki wake pindi alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kabishe akitangaza mshindi wa tuzo Msanii Bora wa Bongo Flava.
KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
AU
BOFYA HAPA
VIDEO ZAIDI ZINAKUJA
KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
AU
BOFYA HAPA
VIDEO ZAIDI ZINAKUJA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...