Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a "Mzee wa Mtaa kwa Mtaa" wa Kampuni ya Michuzi Media Group juzi kati alitinga ndani ya Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,zilizokuwa zikitolewa katika ukumbi wa maraha na burudani pale Mlimani City,Jijini Dar.
Alichokifanya mwanalibeneke huyo Othman Michuzi kwa kutumia kamera yake
au Jicho Kubwa lionalo mbali,ni kurekodi matukio mbali mbali ya usiku huo zikiwemo video za matukio,ambapo video hizo zinawezekana zikawa ndio tiketi ya kuupeperusha muziki wa Tanzania katika masoko
ya kimataifa, labda wengi walistushwa na kiwango cha juu cha kimataifa katika video
hii https://www.youtube.com/watch?v=ZDcmpDoZQZM
Wataalamu wa masoko wa kimataifa waliotazama video hiyo katika Youtube,wameshauri kuwa itakuwa jambo la busara kwa Kampuni ya Michuzi Media Group,
Kuhifadhi haki yake katika video hizo, na mameneja wa wasanii au bendi wakae
meza moja na menejmenti ya Michuzi Media Group,ili wakubaliane kutumia
Bidhaa hiyo kuwa Demo ya kuwapromoti wasanii au bendi zao Duniani.
Kuzitumia bila ya ridhaa ya aliepiga video hizo ni kinyume cha sheria.
Kukopi na kupesti bila ya Idhini au ridhaa ya walipiga video hiyo ni kuvunja
sheria na heshima.
ni Ushauri tu,
lakini Hongera nyingi sana sana kwa Mpiganaji Othman Michuzi kutoka kwa wadau wa ughaibuni,kwani Kazi aliyoifanya imeipeperusha vyema Bongo yetu Kimataifa endelea kwa kasi hiyo hiyo
https://www.youtube.com/watch?v=lZYxySYLmI
Unaweza tembelea libeneke lake kwenye link hiyo http://othmanmichuzi.blogspot.com
Pia unaweza tembelea ukurasa wake wa youtube kwa link hii https://www.youtube.com/user/Michuzijr2?feature=watch ili kuona video mbali mbali.
Mdau Msema Kweli
Ughaibuni.
Huyu Dogo kumbe ni simba mwenda pole
ReplyDeletendiye anayekula nyama ! clip zake babu kubwa jamaa ameifanya kazi,muziki wa Tanzania kaupeperusha
Dogo sio mchezo jicho lake kubwa,kadungua
ReplyDeletePia dada yetu Saida Karoli inabidi aimbe nyimbo zake kwa Kiswahili cha lafudhi Kihaya inafwati pia aendeleea na mirindimo ya ala za Kihaya kabisa ili kupanua soko lake la aina ya sanaa anayoifanya vizuri kabisa.
ReplyDeleteHuyu dogo naye kazana usibweteke kumbuka Ankal yupo katika fani karibia miaka 35 , hivyo usiridhike na sifa hizi.