Hapa ni kwenye Mataa ya kuongozea magari,Ilala Boma na taa zinaonekana ni nyekundu kuzuia magari ya upande mmoja kupita ili kuruhusu ya upande mwingine,lakini hawa jamaa wa boda boda wanapita kana kwamba taa hizo wao haziwahusu,na ukiangalia pembeni pale upande wa kushoto kuna Askari Polisi kikosi maalum cha Usalama barabarani lakini nao wanaangalia tu.kikweli swala hili si la kufumbiwa macho hata kidogo na hatua za haraka zichukuliwe juu ya wahusika hawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2013

    Kwa sheria ya bararani hapa Bongo bodaboda na baiskeli zinaruhusiwa kuvuka taa nyekundu zikiona kuna mwanya wa kufanya hivyo. Ndio maana askari wa usalama barabarani hawawazuii. Ila ikitokea kwa bahati mbaya bodaboda ikasababisha ajali basi itakuwa imekula kwake

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2013

    Hao jamaa mjomba kila nchi, nenda India, Uganda kote ni balaa. rwanda nadhani wanajitahidi sana kwa sababu wote wanavaa vest zinazonesha usajili wao na sheria inawapa adhabu kali sana kama wakiikiuka

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2013

    Bodaboda nyingi ni za matrafiki hivyo ndoi maana wala hawazioni kama zinavunja sheria. Lakini wanadanganyika hawa wabodaboda.Zinawamaliza kama nini!

    Alimradi wao matrafiki wanaingiza siku hizo ajali haziwahusu. Lakini wajinga ndio waliwao

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2013

    maana ya bodaboda ni wahi kufika hivyo nyie msio na haraka shangaeni ktk mataa.
    Mdau
    Mhangaikaji

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2013

    Hawa jamaa sasa ndiyo wamekuwa simba wa mjini, wanaogopwa sana na kila mtu hapo walipo wana silaha like VISU, Jambia na mapanga. Kila mtu anatumia msemo kuwa Funika kombe mwanaharamu apite. Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2013

    kila kibopa au fisadi wa serikali yetu anazo hizo bodaboda kama 10 zinaleta hela ya kuongezea mboga nyumbani

    je? ni sheria gani zitachukuliwa?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2013

    Nakubaliana na mwandishi, hata polisi wachukuliwe hatua kwa uzembe huo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...