Hapa ni kwenye Mataa ya kuongozea magari,Ilala Boma na taa zinaonekana ni nyekundu kuzuia magari ya upande mmoja kupita ili kuruhusu ya upande mwingine,lakini hawa jamaa wa boda boda wanapita kana kwamba taa hizo wao haziwahusu,na ukiangalia pembeni pale upande wa kushoto kuna Askari Polisi kikosi maalum cha Usalama barabarani lakini nao wanaangalia tu.kikweli swala hili si la kufumbiwa macho hata kidogo na hatua za haraka zichukuliwe juu ya wahusika hawa.
Home
Unlabelled
SWALA LA HAWA JAMAA WA BODA BODA KUVUNJA SHERIA BARABARA HATA SI LA KUFUMBIWA MACHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kwa sheria ya bararani hapa Bongo bodaboda na baiskeli zinaruhusiwa kuvuka taa nyekundu zikiona kuna mwanya wa kufanya hivyo. Ndio maana askari wa usalama barabarani hawawazuii. Ila ikitokea kwa bahati mbaya bodaboda ikasababisha ajali basi itakuwa imekula kwake
ReplyDeleteHao jamaa mjomba kila nchi, nenda India, Uganda kote ni balaa. rwanda nadhani wanajitahidi sana kwa sababu wote wanavaa vest zinazonesha usajili wao na sheria inawapa adhabu kali sana kama wakiikiuka
ReplyDeleteBodaboda nyingi ni za matrafiki hivyo ndoi maana wala hawazioni kama zinavunja sheria. Lakini wanadanganyika hawa wabodaboda.Zinawamaliza kama nini!
ReplyDeleteAlimradi wao matrafiki wanaingiza siku hizo ajali haziwahusu. Lakini wajinga ndio waliwao
maana ya bodaboda ni wahi kufika hivyo nyie msio na haraka shangaeni ktk mataa.
ReplyDeleteMdau
Mhangaikaji
Hawa jamaa sasa ndiyo wamekuwa simba wa mjini, wanaogopwa sana na kila mtu hapo walipo wana silaha like VISU, Jambia na mapanga. Kila mtu anatumia msemo kuwa Funika kombe mwanaharamu apite. Kazi kweli kweli
ReplyDeletekila kibopa au fisadi wa serikali yetu anazo hizo bodaboda kama 10 zinaleta hela ya kuongezea mboga nyumbani
ReplyDeleteje? ni sheria gani zitachukuliwa?
Nakubaliana na mwandishi, hata polisi wachukuliwe hatua kwa uzembe huo.
ReplyDelete