Na Geofrey Tengeneza.
Nyota ya Tanzania katika sekta ya Utalii imeendelea kung’ara zaidi badaa ya hivi karibuni kuchaguliwa kuwa ndio nchi bora kwa watu mbalimbali kuweza kufanya safari za kitalii miongoni mwa nchi barani Afrika.
Kwa mujibu utafiti uliofanywa na kutolewa hivi karibuni na katika mtandao wa Kampuni ya marketplace kwa ajili ya safari za Africa (marketplace for African safari tour)
Tanzania imepata kura nyingi zaidi ziliyotolewa kama maoni ya watu kufuatia utafiti huo ambapo Safaribooking .com ilifanya mchanganuo huo kwa kupitia maoni 3061ya zaidi ya watalii na wasafiri waliohusishwa katika utafiti huo na kuhitimisha kuwa katika nchi zote zilizopendekezwaa barani Africa,Tanzania ni zaidi.
Tanzania imekuwa ya kwanza kwa kupata wastani wa alama 4.8 kwa nchi tano mashuhuri barani Africa kati ya nchi nane zilizoshiriki. Botswana na Kenya zilipata wastani wa alama 4.7 kila moja zikifuatwa na Africa kusini na Zambia zilizopata wastani wa alama 4.6 kila moja dhidi ya Namibia iliyopata wastani wa 4.5 na Uganda kupata wastani wa 4.2 dhidi ya Zimbabwe iliyopata 4.2
Kama nchi bora kwa safari za kitalii baran Africa, Tanzania ikitazamwa pia kama lango bora
Miongoni mwa sababu kubwa zinazotajwa kuchangia ushindi wa Tanzania ni pamoja na baadhi ya vivutio vyake yake maarufu kama Hifadhi ya Taifa Serengeti na Kreta ya ngorongoro ambavyo vimekuwa vikivutia watalii wengi kuja kutoka sehemu mbalimbali Duniani. Serengeti ni makazi ya uhamiaji mkubwa ambapo wanyama kama pundamilia na nyumbu huhama, alisema Wouter Vergeer mmiliki wa tovuti huko nchin Netherland.
“Anaongeza kuwa wasafiri na wageni wameipigia kura Tanzania kwa kuwa na sokwe wengi Afrika na kwa kupokea wageni ambao huja kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika mlima Kilimnajaro, na pia wageni hufurahia uhalisia wa wanyama mwitu . Kuna uchaguzi huru wa safari kwa bajet yoyote na mapumziko ya furaha katika kisiwa cha Zanzibar. Safari ni rahisi kwa ndege katika kukamilisha mzunguko huo. Tanzania pia ni nchi iliyo imara kisiasa na kiusalama”
Akiongea na Safaribooking alisema anashangaa kuona kuwa watalii wanaweza kuitembeleaTanzania kipindi chochote cha mwaka ikiwemo kipindi cha masika jambo ambalo amesema limeifanya Tanzania kusifiwa na watalii wengi wanaotembelea nchini. Mwandishi wa Six Lonely Planet guides to Africa Bi Mary Fitzpatrick kutoka Marekani, aliwahi kuandika kuwa pamoja na wanyamapori wake na vivutio vingine vizuri Tanzania imejaaliwa kuwa na viumbe wazuri wa kila aina, miti aina ya acacia, mibuyu na mingine mingi ambavyo vyote vinapamba sura ya nchi, na kuifanyaTanzania ni nchi bora kwa safari Africa.
Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kung’ara barani katika sekta ya utalii kwani itakumbukwa kuwa mwezi Februari mwaka huu Tanzania iliweka rekodi ya aina yake pale vivutio vyake vyote vitatu vya Tanzania vilivyoingia katika shindano la kutafuta Maajabu Saba ya Asili Barai Afrika ambavyo ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (kwa maana ya nyumbu wahamao), Mlima Kilimnjaro na Kreta ya Ngorongoro vilishinda na kuwa miongoni mwa maajabu Saba ya Asili ya Afrika huku Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiongoza kwa kupigiwa kura nyingi zaidi..JPG)
Baadhi ya watalii wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujioea wanyama mbalimbali ikiwemo makundi ya nyumbu wakati yakivuka mto Mara kurejea katika hifadhi hiyo kutoka Maasai Mara.
Hongera Tanzania !!!
ReplyDeleteHapo bado kabisa tunahitaji kuzidisha sana zaidi ya sifa hizo tulizopewa, tunao uwezo mkubwa sana wa kufika mbali kwa Utalii peke yake.
Tunahitaji maboresho zaidi kwa:
1.TUKATAE ''SINGLE TOURISM VISA'' YA AFRIKA YA MASHARIKI:
TUFIKIRIE ZAIDI KUHUSU KAMPENI ZA NDUGU ZETU WA AFRIKA YA MASHARIKI WANAOTAKA 'SINGLE TOURISM VISA', NI KUWA KENYA,UGANDA RWANDA NA BURUNDI WAMESHAONA TANZANIA INAFUNIKA SANA, ''''LICHA YA KAMPENI CHAFU ZA KENYA ZA KUTUSHUSHA NA KUTUHARIBIA MIAKA NENDA MIAKA RUDI HATIMAYE TUMEWEZA KUWA JUU ZAIDI YAO!.
HAWA HASA KENYA WANATAKA SANA HII KITU 'SINGLE TOURISM VISA' YAANI MTALII AKIINGIA KTK AFRIKA YA MASHARIKI ANATEMBELEA NCHI ZOTE (5) TANO KWA VISA MOJA, NI KUWA
(i)WANATAKA KUTUMIA SIFA ZETU ZA UBORA WA VIVUTIO VYETU KUNUFAIKA KIBIASHARA, NI ''''MUHIMU TUKATAE SUALA LA 'SINGLE TOURISM VISA'
(ii)KWA SABABU ''SINGLE TOURISM VISA'' LITASHUSHA MAPATO YETU NA UWEZO WETU KIUSHINDANI.
(iii)''SINGLE TOURISM VISA'' ITAATHIRI AJIRA YA WATANZANIA KTK SEKTA YA UTALII.
(iv)'SINGLE TOURISM VISA' ITAHATARISHA UDHIBITI WA VIVUTIO VYETU NA KURUHUSU HUJUMA DHIDI YETU KIRAHISI KWA KUWA NDUGU ZETU WASIO AFRIKA YA MASHARIKI HASA KENYA NIA SIO NJEMA NA WASIO WAAMINIFU WANAWEZA KUUTUMIA MWANYA HUO VIBAYA...MFANO WALIVYO LAZIMISHA KUUFUNGUA MPAKA WA MBUGANI ULIOFUNGWA MWAKA 1977 BAADA YA AFRIKA MASHARIKI YA KWANZA KUVUNJIKA, MPAKA HUO UKIFUNGULIWA TUTAATHIRIKA VIBAYA SANA...NI VEMA TUKATAE KATA KATA USIFUNGULIWE KABISA.
(v)TUNAHITAJI KUTUMIA SIFA HIZI KUBORESHA ZAIDI UWEZO WETU KIBIASHARA ,KIHUDUMA KWA WAGENI WA UTALII NA NAFASI YA USHINDANI DHIDI YA MAJIRANI ZETU WABAYA HASA KENYA.
JANJA YENU KWISA JUA KENYA WANATAKA KUSAFIRIA NYOTA YETU INAYONG'ARA....BOTSWANA ILIKATAA 'SINGLE TOURISM VISA' NA SOUTH AFRIKA KWA SABABU HIZO TANO (5) NINAZOSEMA HAPO JUU.
Tatizo wanasiasa matumbo mbele.Sababu nyingine ni amani yetu ndo maana tunahitaji tukatae katkata wanasiasa wanaotafuta kukaa madarakani kwa nguvu zote.Tena hatuna huruma na amani yetu hasa kwa yanayozidi kujiri dhidi ya CCM na CHADEMA wakiendelea hatuna budi kushinikiza vifutiwe usajiri kwani nchi ni yetu na si ya vyama.tuko tayari hata kuwa na Lipumba wetu kuliko vyama vyenye chokochoko
ReplyDelete