Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.
Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Mergitu Ebba akiwanoa waandishi wahabari waliohudhuria semina hiyo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji



Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.

Mkufunzi huyo amesema kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia ndani ya jamii vinaweza kumalizwa endapo Wanahabari watafanya kazi ya kujitolea ya kuibua na kuiambia jamii madhara ya vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya jamii ya Mbeya inasadikika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba Mfuko wa raisi wa Marekani umetoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha Vitendo hivyo vinaisha ambapo msaada huo utalenga Nchi tatu ikiwemo Tanzania.

Amesema Nchini Tanzania ni Mikoa minne  itakayohusika  ambayo ni Mbeya, Iringa, Mara na Dar Es Salaam ambapo kwa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya Sita zitakazohusika ambazo ni Mbeya Jiji, Ileje, Kyela, Rungwe, Busokelo na Mbeya Vijijini.

Na Mbeya yetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2013

    Huu hasa ni Ukoloni wa kutupa! TGNP, TAMWA, WILAC, TAWLA wapo na wanafanya kazi nzuri tangu miaka 30 iliyopita. Kazi hii hii ya kuwezesha kukomesha masuala ya unyanyasaji Kijinsia. Leo hii Mmarekani Walter Reeds .... anachokisema kipya mbali na pesa yake ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...