Picha na habari naa Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii,Moshi
MTU mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki Dunia
huku wengine sita wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea
juzi usiku majira ya saa moja katika eneo la Kawawa wilayani Moshi.
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC
muda mchache baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha magari
mawili likiwemo basi la abiria lijulikanalo kwa jina la Metro ambayo
yaligongana uso kwa uso na Loli aina ya Fuso lililokuwa likielekea Dar
es salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ilitokea baada ya
dereva wa gari aina ya Fuso kujaribu kulipita Loli jingine aina ya
Scania likiwa na trela lake kabla ya kukutana na basi la Metro
lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha ndipo magari hayo
yakagongana uso kwa uso.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alithibitsha kutokea
kwa ajali hiyo huku akitaja namba za usajili wa magari yalihusika
katika ajali hiyo kuwa ni basi la Metro aina ya Yutong lenye namba za
usajili T 129 BQL likiendeshwa na Oscar na Fuso lenye namba za
usajili T 615 AWB lililokuwa likiendeshwa na Goodluck
Aseri.(45)lilikuwa likitokea Moshi kuelekea Njia panda Himo.
Kamanda Boaz alisema Dereva wa basi aliyefahamika kwa jina moja la
Oscar alifariki dunia papo hapo huku kondakta na abiria wengie watano
katika basi hilo walipata matibabu katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Alisema jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Dereva wa
Fuso kwa maelezo zaidi na kwamba mara uchunguzi utakapokuwa
umekamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za usalama
Barabarani.
Muonekano wa mbele wa gari aina ya Fuso baada ya kugongana uso kwa uso na basi a Metro baada ya kile kilichosemekana kuwa ni kupata hitilafu katika mfumo wa breki.
Gari aina ya Fuso ikipakia mizigo iliyokuwa katika gari lililopata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Metro na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Sehemu ya mabaki ya gari aina ya Fuso.
Dereva wa Fuso aliyefahamika kwa jina la Goodluck Aseri akiwa amelazwa katika hospitali ya KCMC akiwa na pingu mkononi.
Kila barabara zikijengwa katika kiwango cha lami ndiyo ajali zinazidi kuongezeka.
ReplyDeleteInaonyesha dhahiri kwamba tumezoea 'vya kunyonga' vile 'vya kuchinja' hatuviwezi.
Hii ndio vita yetu watanzania,tunakwisha tu, ukipiga mahesabu ya waliopotezana wanaopoteza maisha kwa ajali za barabarani yawezekana ukapata idadi sawa na idadi ya wanaofariki ktk civil war.
ReplyDeleteThat is really humiliation, you get an accident and they tie you to a bed. Is that really a hospital? Should be sent to India or SA where the ruling class go, am serious!
ReplyDeletevibaya sana wanavyofanya . Mtu amepata ajali si kwa uzembe ila ni matatizo kwenye mfumo wa break.
ReplyDeleteHapa najiuliza hawa wafunga pingu wana akili kweli?
Lakini siwalaumu sana kwa sabb mswahili akinyanyuka hapo , nduki wala hasubiri kutoa maelezo.
bongo tambarare! sirudi ng'o!
ReplyDelete