Ankal salaam.

Naomba uniulizie wadau wako, hivi haya mawe meupe yanayoonekana kwa wingi sana pembezoni mwa kipande cha barabara kati ya Segera na Mkata, yana matumizi gani???

 Nauliza hivi kwa kuwa wahusika walianza kidogo kidogo kuyakusanya kwa kutumia "visalfeti" au malboro na kuuza kwa waliojua matumizi yake, lakini kwa sasa ukipita utakuta yamerundikwa kwa kiasi kikubwa sana na zipo semi-trela zinapakia kwa wingi.

 Ni mawe mazuri ajabu, meupe na yenye kumetameta wakati jua likiwa kali sana. Jamani mwenye kujua matumizi yake tafadhali atujuze ili tuyachangamkie mapema kabla "wawekezaji" toka urusi au uchina hawajayavamia.

 Wkend njema.
 Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2013

    Tunapozungumzia ujasiliamali hapo ndio tunapima uwezo wetu wa kitanzania katika swala Zima la uvumbuzi na ugunduzi. Sasa wewe badala ya kuumiza kichwa kufikiria nini cha kufanya na hayo mawe matokeo yake unataka kutafuniwa kila kituna ndio maana unaogopa wawekezaji. Kuwa mbunifu mdau na hivyo ndivyo maendeleo huja. Usitegemee kufanyiwa na watu ili upate mafanikio. Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2013

    Mdau hayo mawe yanaitwa ''TANGA STONE''.

    Moja ya matumizi yake yanatumika kuwekea Urembo kwenye nyumba kama inavyofanywa Gypsum.

    Kama unavyoona yna metameta yakiwekwa ndani ya nyumba ama nje inakuwa ni mojawapo ya kuipa nyumba hadhi ya juu.

    Kazi kwako Mdau, fanyia uchangamkaji kwaupande wako wakija hao Warusi na Wachina wewe ndio unawabana ktk Biashara!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2013

    Mawe hayo ni ''Tanga Marble'' ama Tanga Stones' ynatumika kwa njia nyingi lakini kuweka urembo kwenye nyumba.

    Yanaweza kuwekwa ukutani ndani, nje ama kutumika katika simenti sakafuni chini.

    Kokoto zake ama changarawe zake ni urembo wa nyumba pia ama zinatumika kama material za kuweka urembo mijengoni.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2013

    Mdau hayo ni mawe ya bahati!
    ...................................

    Hapana Mdau, usije ukapata Imani potofu bureee, mawe yanatumika kwa Ujenzi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2013

    mawe yanasagwa na kuwa chokaa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2013

    YALE HUTUMIKA KUTENGENEZEA CHOKAA NA GYPSUM

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2013

    Yanatengenezea chokaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...