.jpg)
Afya njema
na kula vizuri ni mambo muhimu kwa kila mtu, na ni jambo muhimu zaidi la kuzingatia
katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kuna watu
wanadhani Ramadhani ni wakati wa kuunda upya matumbo na miili yao na kupumzika. Yaani baada
ya kufunga kula na kunywa kutwa nzima wanadhania wanahitaji kula chakula kingi
ili kufidia walichokosa mchana. Hii ianweza kuwa tabia isiyo njema kiafya.
Watu
wengine hudhania ni haki yao kula kupindukia kila jioni wakati wa kufuturu kwa
kuwa ilikuwa siku ndefu iliyopita bila kitu kupita kinywani. Ni kweli kwamba
kila futari ni sherehe, lakini pia si uwongo kwamba ni muhimu usile chakula
kupindukia hadi kuvimbilwa, ama usile
chakula kisicho chema kiafya
Kaa
ukielewa kuwa kutapanya ama kupoteza ama kufuja chakula ni pamoja na kula
kuliko unavyohitaji, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa kufuturu.
Elewa kwamba wakati wa kufuturu, moja ya tatu la tumbo lako ni kwa ajili ya
chakula, moja ya tatu ingine ni kwa ajili ya maji na moja ya tatu ingine ni kwa
ajili ya hewa.
Kama
unafakamia futari kupita kiasi wakati wa kufuturu, ni wazi utanenepeana na
kuongezeka uzito wakati wa Ramadhani, hivyo kukosa afya njema. Nguzo hiyo
muhimu (kufunga) kwa Uislamu ni mojawapo ya njia kuu za kukufanya ubakie msafi
na mwenye afya bora na si kinyume chake, kwani mwili wako ni dhamana kubwa kutoka
kwa Mwenyezi Mungu. Inakulazimu uheshimu maumbile yako kama alama ya kumuabudu
Allah. Na ili kuweka mwili wako vyema na kuheshimu zawadi hiyo toka kwa Mola,
inabidi ufuate yafuatayo:
• Jitahidi
sana kula vyakula vyenye kuleta afya wakati wa kufuturu
– Ni vyema
wakati wa Ramadhani ukala vyakula, mboga mboga na matunda kwa wingi kama
ufanyavyo wakati wote wa mwaka. Wakati wa kufuturu nusu ya futari yako iwe
matunda na mboga mboga. Hii itakusaidia kupata lishe bora, kusikia njaa kiasi
mchana, na pia epukana na kuvimbilwa, katika misingi ile ile ya kutunza mwili
wako kama njia ya kumtukuza Mola kwa zawadi ya mwili aliokupa
– Futari
aghalabu huwa ni chakula cha kukaangwa, hivyo jaribu kupunguza kula vyakula
vyenye mafuta mengi. Yaani kula kwa kiasi vyakula vya kukaangwa, halwa,
mafuta katika nyama pamoja na mafuta katika ubwabwa na mboga.
–Jaribu
kupunguza idadi ya tende unazokula kila siku. Zisizidi nne. Tende zina sukari
nyingi mno pamoja na kalori (calories), kama peremende vile
– Usiweke
vijiko zaidi ya viwili vya sukari kwenye kikombe chako cha uji ama chai.
– Usiongeze sukari kwenye juisi yako
– Usiongeze sukari kwenye juisi yako
–Jizuie
kula vitafunwa vyenye sukari tele kama vile keki, ice cream, halwa na visheti
ama kashata. Hivyo viweke hadi siku ya
sherehe za Iddi, na sio kula kila siku.
• Kunywa maji mengi.
– Maji ni yenye afya zaidi kuliko soda, juisi ama vinywaji
vingine vyenye sukari.
– Maji yatakusaidia ujisikie poa kutwa nzima, kwani hicho si kirutubisho tu bali pia ni kiyeyushi chema cha chakula tumboni mwako.
– Maji yatakusaidia ujisikie poa kutwa nzima, kwani hicho si kirutubisho tu bali pia ni kiyeyushi chema cha chakula tumboni mwako.
MJADALA AMA
USHAURI ZAIDI UNAKARIBISHWA


.jpg)

Haifai kula kupindukia, iwe Mwezi wa Ramadhani au hata siku za kula mchana. Katika Uislam tunatakiwa kula kwa kuligawa tumbo katika "Theluthi Tatu" yaani 1/3, moja ya Chakula, ya pili ya Maji na ya tatu ya hewa (iwe tupu ili uweze kupumuwa vizur)i. Sasa unamkuta mtu kala mpaka pa kupumulia hana, anagaragara tu kwa shibe, haifai namna hiyo, mwisho raha yote ya chakula inageuka karaha. Nawatakia RAMADHAN MOUBARAK.
ReplyDeleteahsante kwa taarifa
ReplyDeletewaacheni watu wajimwage jamani!!kaaa!!siku sio nyingi hizo!!watafanya diet baadaye!!raha jipeni wenyiwe wenzangu waislamu!!
ReplyDeleteInshaallah kwa elimu hiyo!
ReplyDeleteHahahahaha!
ReplyDeleteSamahani naanza kwa kuecheka ingawa Mada ni yenye maneno mazuri sana.
Ahsante Mtoa Makala umetusaidia sana, Nieanza kwa kucheka maana nimekumbuka ktk Facebook Wadau waliwahi kuweka picha ya Muumin aliyemeza FUTARI hadi akwawa amelala chali na kupumua hawezi!
Sasa matokeo yake mtu anapokula kupita kiasi anaweza kushindwa hata kutekeleza Ibada mfano Swala ndefu ya Taraweihy.
Duuu Mdau umepiga Pentagoni!
ReplyDeleteMaana wengi wanafikiri kufuturu ni kula kupita kiasi, ama wengine wanadhani kula sana Futari au Daku kunaweza kupunguza Swaumu siku inayofuata kitu ambacho sio kweli!
Mfano ukila sana chakula kama Pilau au wali wenye mafuta mengi ktk Futari au Daku matokeo yake sikuinayofuata Swaumu huwa kali zaidi kwa kuwa utakuwa na Kiu kali sana, ieleweke ktk Swaumu iliyo kali zaidi ji ya kiu ya maji zaidi ya chakula.
Waumini tusile Futari na Daku kupita kiasi, tule kawaida tu.
Nani aliwaambia Swaumu inaweza kukatiwa Denge?
Ulafi ni Hali ya kula kupindukia. Ni dhambi pia. Iwe mfungo au la, ni tabia mbovu inayooambatana na dhambi nyinginezo Kama uvivu, tamaa, uwongo na uchoyo. Mungu hapendezeshwi na tabia hizi. Kula hakuna mwisho ni Kama kulala, kuamka, kwenda haja. Ni mambo mtambuka katika maisha ya mwanadamu ye yote aliye hai. Ni kifo tu mambo haya hukoma. TAFAKARI
ReplyDelete