Afya njema na kula vizuri ni mambo muhimu kwa kila mtu, na ni jambo muhimu zaidi la kuzingatia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kuna watu wanadhani Ramadhani ni wakati wa kuunda upya  matumbo na miili yao na kupumzika. Yaani baada ya kufunga kula na kunywa kutwa nzima wanadhania wanahitaji kula chakula kingi ili kufidia walichokosa mchana. Hii ianweza kuwa tabia isiyo njema kiafya.
Watu wengine hudhania ni haki yao kula kupindukia kila jioni wakati wa kufuturu kwa kuwa ilikuwa siku ndefu iliyopita bila kitu kupita kinywani. Ni kweli kwamba kila futari ni sherehe, lakini pia si uwongo kwamba ni muhimu usile chakula kupindukia hadi kuvimbilwa,  ama usile chakula kisicho chema kiafya
Kaa ukielewa kuwa kutapanya ama kupoteza ama kufuja chakula ni pamoja na kula kuliko unavyohitaji, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa kufuturu. Elewa kwamba wakati wa kufuturu, moja ya tatu la tumbo lako ni kwa ajili ya chakula, moja ya tatu ingine ni kwa ajili ya maji na moja ya tatu ingine ni kwa ajili ya hewa.
Kama unafakamia futari kupita kiasi wakati wa kufuturu, ni wazi utanenepeana na kuongezeka uzito wakati wa Ramadhani, hivyo kukosa afya njema. Nguzo hiyo muhimu (kufunga) kwa Uislamu ni mojawapo ya njia kuu za kukufanya ubakie msafi na mwenye afya bora na si kinyume chake, kwani mwili wako ni dhamana kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Inakulazimu uheshimu maumbile yako kama alama ya kumuabudu Allah. Na ili kuweka mwili wako vyema na kuheshimu zawadi hiyo toka kwa Mola, inabidi ufuate yafuatayo:
 • Jitahidi sana kula vyakula vyenye kuleta afya wakati wa kufuturu
– Ni vyema wakati wa Ramadhani ukala vyakula, mboga mboga na matunda kwa wingi kama ufanyavyo wakati wote wa mwaka. Wakati wa kufuturu nusu ya futari yako iwe matunda na mboga mboga. Hii itakusaidia kupata lishe bora, kusikia njaa kiasi mchana, na pia epukana na kuvimbilwa, katika misingi ile ile ya kutunza mwili wako kama njia ya kumtukuza Mola kwa zawadi ya mwili aliokupa
– Futari aghalabu huwa ni chakula cha kukaangwa, hivyo jaribu kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi. Yaani   kula kwa kiasi vyakula vya kukaangwa, halwa, mafuta katika nyama pamoja na mafuta katika ubwabwa na mboga.
• Punguza kula vyakula vyenye sukari nyingi wakati wa Ramadhani
–Jaribu kupunguza idadi ya tende unazokula kila siku. Zisizidi nne. Tende zina sukari nyingi mno pamoja na kalori (calories), kama peremende vile
– Usiweke vijiko zaidi ya viwili vya sukari kwenye kikombe chako cha uji ama chai.
– Usiongeze sukari kwenye juisi yako
–Jizuie kula vitafunwa vyenye sukari tele kama vile keki, ice cream, halwa na visheti ama kashata. Hivyo viweke hadi  siku ya sherehe za Iddi, na sio kula kila siku.
• Kunywa maji mengi.
– Maji ni yenye afya zaidi kuliko soda, juisi ama vinywaji vingine vyenye sukari.
– Maji yatakusaidia ujisikie poa kutwa nzima, kwani hicho si kirutubisho tu bali pia ni kiyeyushi chema cha chakula tumboni mwako.
MJADALA AMA USHAURI ZAIDI UNAKARIBISHWA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Haifai kula kupindukia, iwe Mwezi wa Ramadhani au hata siku za kula mchana. Katika Uislam tunatakiwa kula kwa kuligawa tumbo katika "Theluthi Tatu" yaani 1/3, moja ya Chakula, ya pili ya Maji na ya tatu ya hewa (iwe tupu ili uweze kupumuwa vizur)i. Sasa unamkuta mtu kala mpaka pa kupumulia hana, anagaragara tu kwa shibe, haifai namna hiyo, mwisho raha yote ya chakula inageuka karaha. Nawatakia RAMADHAN MOUBARAK.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2013

    ahsante kwa taarifa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2013

    waacheni watu wajimwage jamani!!kaaa!!siku sio nyingi hizo!!watafanya diet baadaye!!raha jipeni wenyiwe wenzangu waislamu!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2013

    Inshaallah kwa elimu hiyo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2013

    Hahahahaha!

    Samahani naanza kwa kuecheka ingawa Mada ni yenye maneno mazuri sana.

    Ahsante Mtoa Makala umetusaidia sana, Nieanza kwa kucheka maana nimekumbuka ktk Facebook Wadau waliwahi kuweka picha ya Muumin aliyemeza FUTARI hadi akwawa amelala chali na kupumua hawezi!

    Sasa matokeo yake mtu anapokula kupita kiasi anaweza kushindwa hata kutekeleza Ibada mfano Swala ndefu ya Taraweihy.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2013

    Duuu Mdau umepiga Pentagoni!

    Maana wengi wanafikiri kufuturu ni kula kupita kiasi, ama wengine wanadhani kula sana Futari au Daku kunaweza kupunguza Swaumu siku inayofuata kitu ambacho sio kweli!

    Mfano ukila sana chakula kama Pilau au wali wenye mafuta mengi ktk Futari au Daku matokeo yake sikuinayofuata Swaumu huwa kali zaidi kwa kuwa utakuwa na Kiu kali sana, ieleweke ktk Swaumu iliyo kali zaidi ji ya kiu ya maji zaidi ya chakula.

    Waumini tusile Futari na Daku kupita kiasi, tule kawaida tu.

    Nani aliwaambia Swaumu inaweza kukatiwa Denge?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2013

    Ulafi ni Hali ya kula kupindukia. Ni dhambi pia. Iwe mfungo au la, ni tabia mbovu inayooambatana na dhambi nyinginezo Kama uvivu, tamaa, uwongo na uchoyo. Mungu hapendezeshwi na tabia hizi. Kula hakuna mwisho ni Kama kulala, kuamka, kwenda haja. Ni mambo mtambuka katika maisha ya mwanadamu ye yote aliye hai. Ni kifo tu mambo haya hukoma. TAFAKARI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...