Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph (katikati) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wanafunzi na walimu wakifanya usafi katika mazingira ya shule ya msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katika kati ya jiji la Dar es Salaam.
Mkusanyaji wa Mapato wa kampuni hiyo Bw. Almachlus Rwakatale akikabidhi jumla ya ndoo 16 za rangi kwa Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya. Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph.
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph na Mkuu wa mazingira katika Shule ya Msingi ya Bunge ya jijini Dar es Salaam Mwl. Frida Madanganya wakishirikiana kumwagilia maji moja ya miti waliyopanda katika shule hiyo kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Meneja Muajiri wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro Ltd. Bi. Vidah Joseph akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na ratiba wanazozifanya kila mwaka za utaratibu wa kuweka mazingira ya manispaa ya Ilala katika hali ya usafi ikizingatiwa ni katikati ya jiji la Dar es Salaam na safari hii wametoa ndoo 16 za rangi katika Shule msingi Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...