Na Abdulaziz Video, Lindi
Halmashauri ya wilaya ya Lindi, inaandaa taratibu za kuiburuza
Mahakamani Gereji ya Auto Works Service ya Jijini Dar es salaam,kwa
madai ya kuendelea kuishikilia gari yake, huku tayari ikiwa imeshalipwa
fedha zote zilizokuwa ni ghalama za matengenezo yake.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Grace
Mbaruku,katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani,lililofanyika
hivi karibuni .
Mbaruku ametoa kauli hiyo,alipokuwa akijibu baadhi ya maswali kutoka
kwa madiwani hao, waliotaka kufahamu hatua iliyofikiwa juu ya gari lao
aina ya Toyota Cruser STJ 1826 iliyopelekwa gereji hiyo,kwa
matengenezo na kuzuiwa na mzabuni huyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa
akidai alipwe fedha zaidi.
Aliwaambia madiwani hao kwamba gari hiyo ilipelekwa gereji hiyo ya
Auto Works Service kwa gharama ya Sh,19,446,400/-lakini matengenezo
ambayo yamefanyika hadi kutembea yamefikia kiasi cha
Sh,7,038,700/-ambacho tayari kimelipwa kupitia LPO Namba 001167.
“Kama ni fedha za matengenezo tayari ameshalipwa,lakini bado mzabuni
huyu anaendelea kuizuia gari huku akitaka hadi alipwe
Sh,19,446,400/-huku tayari fedha halali kwa kazi iliyofanyika
ameshalipwa,,,,,,,,,,,sijui jeuri hii anaipata kutoka wapi?”Alisema
Mbaruku.
Pia,mkurugenzi huyo mtendaji amesema kutokana na mzabuni huyo
kuendelea kuishikilia gari hiyo hadi alipwe fedha hizo, Yaonesha
anataka kuiibia Halmashauri yake kiasi cha Sh,12,407,700/-ikizingatiwa
tayari imeshamlipa kulingana na kazi aliyokuwa ameifanya.
Mkurugenzi huyo akasema kinachomsikitisha ni pale mzabuni huyo hataki
kuikabidhi gari hilo,kwa madai kuwa bado anaidai fedha Halmashauri
hiyo.
Akasema kutokana na kitendo cha mzabuni huyo kuendelea kuizuia gari
hiyo,uongozi wa Halmashauri umeamua kuwasiliana na mwanasheria wake
ili mzabuni huyo aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Baada ya maelezo hayo,madiwani kwa kauli moja wamemtaka mkurugenzi
huyo,kuharakisha taratibu za kuwasiliana na mwanasheria ili gari hiyo
STJ 1826 likachukuliwe kwa Mwenye gereji hiyo haraka ili kusaidia
shughuli za kiutendaji
Awali diwani wa kata ya Longa,Abdu Mjenga (CCM) aliitaka halmashauri
hiyo kutoa taarifa kwa madiwani kuhusiana na gari hiyo iliyopelekwa
kwenye gereji hiyo kwa muda mrefu bila ya wao kutopatiwa maendeleo na
mrejesho wake huku wakijua imelipiwa matengenezo yake.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Bi. Grace Mbaruku, akiongea katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani,lililofanyika hivi karibuni .
Mmoja wa madiwani akichangia katika baraza hilo
Nyie mliingia mkataba wa 19m sasa mnataka kulipa 7m tu!, nyie watu wa Lindiwakati mnasaini mkataba hakuwa mnajua kusoma? Acheni utapeli,
ReplyDeletehivi kweli hata mhandisi wenu ameshindwa kuwashauri kwenye hilo suala mpaka mnajianika kijinga namna hii
Hivi huyu Mkurugenzi anachekesha kweli... hivi kwa miaka mitatu walikuwa wapi kuchukua hatua za kisheria?
ReplyDeletePoleni sana waheshimiwa.
ReplyDeleteBut I think you should first of all take the person who designed your robes of office to court.For intentionally or with tongue in cheek made the robes make you appear like harlequins.
very good majoho, wamependeza kweli!!
ReplyDeleteYaani ni lazima kuvaa hayo makofia; mnatisha!
ReplyDeleteIko kazi - waheshimiwas madiwani - geeee I am shocked by those robes!
ReplyDelete