.Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mkuu mpya ya UNAMID Luteni Jenerali Paul Ignace Mella na kulia ni Luteni Jenerali Wynjones Mathew Kisamba Naibu Kamanda na ambaye pia alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda Mkuu UNAMID. Luteni Jenerali Mella na Luteni Jenerali Kisamba walikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ziara ya Kikazi na mafunzo. Lt. Jenerali Mella anasema yupo tayari kulitekeleza jukumu alilokabidhiwa na Umoja wa Mataifa na kwamba uteuzi wake katika wadhifa huo ni heshima kubwa wa Tanzania, Afrika, kwake yeye binfasi na zaidi kwa JWTZ ambayo mwaka itakuwa inatimizia miaka 50 tangu kuanzishwa kwake
Wageni waalikwa wakipata kitu kidogo.
Mkuu Mpya wa UNAMID Luteni Jenerali Mella akiwa katika picha ya pamoja na waambata wa kijeshi kutoka nchi za Afrika na kwingineko wakati alipotambulishwa kwao katika hafla fupi iliyoandawali na Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. kutoka kushoto ni Naibu Mwakilishi Balozi Ramadhan Mwinyi, Lt. Jenerali Wynjones Kisamba, Balozi Tuvako Manongi, Lt. Jenerali Paul Mella na Maj. Jenerali Ngodi Mkuu wa jeshi la kulinda amani huko Lebano (UNFIL)
mbona huyo hajanyonga mjusi!
ReplyDelete