Mpigapicha na Mhazini wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) , LEAH SAMIKE anawatangazia kifo cha mume wake Bwana HUMPHREY GEORGE LUPENZA aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lucky  Construction  Limited, (pichani) kilichotokea jana Saa 10: 55 alfajiri katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu tokea Jumapili.

Taratibu za kuaga mwili wa Marehemu zinafanyika mchana wa leo kuanzia saa 6 na nyumbani kwa Marehemu, Kipunguni B -Ukonga Moshi Bar. Jirani na Kanisa la Pentekoste (Kanisa la Mabati) na baada ya Kuaga mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Njombe,kwa Mazishi.

Marehemu ameacha Mke Leah William Samike na watoto 5 ambao ni Maximillian-Samike, Mary -Maria Clara, George, Harrison na Jane-Fatuma.  

Tuungane na familia ya Marehemu katika kuipa faraja.

Humphrey akiwa na Mkewe Leah Samike siku ya harusi yao mara baada ya kula kiapo chao cha ndoa cha kuishi pamoja milele hadi kifo kitakapowatenganisha.

MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2013

    jamani what happened to this handsome man? such a young family man. may lord rest him in peace Amen. poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2013

    AHHHHH!!!!!!!! si kazi ndogo kuondokewa na mume . Mungu wetu amlaze pema peponi ....Amina.

    Pole sana Lupenzas.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2013

    Pole sana Leah, Mungu akutie nguvu ktk kipindi hiki kigumu. anejua contact zao atuwekee hapa ili tuweze kumpa pole

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...