Afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini
Moshi (MUWSA) Dollah Kilo akifurahia jambo na naibu waziri wa maji Dk
Binilith Mahenge wakati akitembelea tangi la maji la kampni ya maji ya
Kiliwater wilayani Rombo.
Tangi la maji la Kampuni ya Kiliwater linalohifadhi maji kwa ajili ya
wakazi wa wilaya ya Rombo.
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipanda katika ngazi ya
tangi la maji la kampuni ya Kiliwater kujionea hali ya ujazo wamji
ikoje katika tangi hilo.
Naibu wziri wa maji Dk Binilith Mahenge akizungumza na watendaji wa
maji wilaya ya Rombo juu ya tangi la maji la kampuni ya Kiliwater.
Naibu wziri wa maji Dk Binilith Mahenge akitizama sehemu ya
kuchanganyia dawa katika tangi la maji la kampuni ya maji la
Kiliwater.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na maji safi mjini Moshi Cyprian
Luhemeje akiongea jambo mbele ya naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge mara baada ya kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya
Rombo.
Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi.
Mhe. Dr. Mahenge kweli kazi anaiweza,
ReplyDeleteMaana wachakachuaji hawaishi Mipango, ukitegemea kupokea taarifa kwa njia za simu utaula wa chuya!.
Wanaweza kupokea Madawa ya kusafishia maji tani 15 kwenye makaratasi wakaandika tani 1.5 halafu mzigo mwingine wanaupeleka huko Miferejini Keko na Manzese.
Mzee mzima hadi anapanda ngazi kuhakikisha?
Mbongo ni kama Kima, ukicheza naye utavuna mabua.
ReplyDeleteNdio maana Mhe. Dr. Mahenge haamini taarifa za kwenye makabrasha hadi apande ngazi ahakikishe mwenyewe!
Ama kweli seeing is believing!
ReplyDeleteNdio maana Kiongozi Dr.Mahenge anapanda ngazi kuhakikisha yeye mwenyewe.
Ama kweli seeing is believing!
ReplyDeleteNdio maana Kiongozi Dr.Mahenge anapanda ngazi kuhakikisha yeye mwenyewe.
Nyinyi mnaparamia kwenye matanki hayo ninyi "Mtaporomoka" humo halafu mkione cha mtema kuni.
ReplyDeletewaziri huyu anafanya kazi sana bila wasiwasi...wangekuwa kumi hivi..tungefika mbali...
ReplyDeleteHapa wachapakazi hawatakiwi bongo. Angalia mashirika ya umma yalikufa kwa sbb wachapakazi aidha walifukuzwa kiaina ama walinyanyaswa wakaacha kazi.
ReplyDeleteNdio maana Tz inaongozwa kiujanja si kisayansi.
Hebu ona.. UCC ya Mlimani ilikuwa murua sana wakati wa Prof. Beda kiutawala. Na uhasibu kulikuwa na mama mmoja jina limenitoka au sikuwahi kulijua.Watu hawa wawili walikuwa wachapa kazi sana.Ndio, kiubinadamu hakuna mkamilifu lakini kampuni ilisonga mbele.
Sijui ni mchawi gani alingilia pale. Prof. wa watu silipofika pale baadaye nikasikia amechimbiwa mkwala akaondolewa. Haya...na huyu mama nikasikia hakutaka kushiriki wizi baada ya prof kuondoka, naye akanyanyaswa ikabidi aachie ngazi.
Hebu ona kampuni inavyoyoyoma kisailensa.