Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo juu ya tozo la kodi katika laini za simu wakati alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Shija – Maelezo)
Na. Eliphace Marwa (MAELEZO)
Serikali yawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na mpango wa ukusanyaji wa kodi ya laini za simu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Mgimwa amesema kuwa Serikali inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kujadili na kupokea mapendekezo kuhusiana na dhamira ya Serikali kutoza kodi kutoka katika laini za simu.
Aliongeza kuwa Serikali ina nia njema ya kuongeza mapato yake ili kuongeza kasi ya kutoa huduma za msingi kwa wananchi wake hususani wa vijijini.
“Lengo hasa la kodi hii ni kuboresha huduma za msingi vijijini kama umeme, maji na barabara ambazo ni duni sana vijijini, hata hivyo tunafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya wananchi na wadau wenye mitazamo mbalimbali” alisema Dk. Mgimwa.
Aidha Dk. Mgimwa amesema kuwa hivi karibuni amekutana na chombo cha watoa huduma za mawasiliano (MoAT) nakujadiliana nao na kuwaahidi kuwa mapendekezo yao yatafanyiwa kazi.
Mkutano huo umekuja baada ya wadau mbalimbali kutoa malalamiko juu ya uwepo wa tozo ya kodi ya laini za simu ambapo mmiliki wa laini ya simu atatakiwa kulipia shilimgi 1000 kila mwezi mara kodi hiyo itakapo anza kutozwa.
Mhe.Dr. Mgimwa,
ReplyDeletelfu halafu Endapo mtaendelea na Msimamo wenu wa Kodi ya Shs. 1,000/= wakati matumizi yangu ndio hayo hayo najaza Tigo Pesa Elfu halafu nahamisha Shs. 200/= ''TENA INAPOBIDI KUPIGA SIMU YA MUHIMU'' wakati wote mimi huwa Nabipu na kupigiwa!
Ama sivyo nitaiweka Simu yangu Darini na Kurudi kwenye maisha ya Ujima!
muhimu kupunguza matumizi yasio kuwa ya msingi kama kununua magari ya serikali ambayo yako kiwango cha juu sana hali ya kuwa serikali bado ni changa.. hata kama kodi itakusanywa kwa kiasi gani haitotosha kwani nchi na viongozi bado ni extravagant.
ReplyDeleteKIKWELI HII SASA INAUMIZA WANANCHI IKIWEMO WAFANYAKAZI,TUNAKATWA KODI KUBWA KUBWA BADO NA VITU TUNAVYOTUMIA PIA TULIPE KODI YANA TUNALIPA MARA MBILI AU ZAIDI,YANI KAMA UNA FAMILIA KILA MWENYE SIMU MZIGO WOTE UNAKUWA WETU SISI WAFANYAKAZI KWELI TUTAISHI VIPI?,SEREKALI IYANGALIE SWALA HILI,WATU KULE KILIMANJARO WANAOFANYA UWEKEZAJI WA KUZALISHA MAUA AWALIPI KODI ATA KIDOGO,MZIGO WOTE KWA MWENYEJI KWELI HII NCHI TUNAENDA WAPI?
ReplyDeleteMawaziri, majaji, wakuu wa mikoa, maofisa wa ngazi za juu serkalini, nk, wote wana land cruiser ya Sh 100,000,000, nyumba ya serikali gharama zote zinalipwa na serikali, wanasafiri business au first class, posho ya safari, nk, .......... What do you expect? Hiyo kodi lazima watatoza na mwaka kesho watapandisha itakuwa Sh 2,000. Watanzania wa kawaida wamelala usingizi. Viongozi wa serikali Tanzania wanaishi dunia tofauti na ile ya watanzania wa kawaida .... Na wanaujua ule msemo ALIYELALA USIMUAMSHE.
ReplyDelete