NA MIZA KONA / HABARI MAELEZO ZANZIBAR
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kulivunja Shirika la Utalii
Zanzibar kutokana na changamoto zinazolikabili Shirika hilo hivi sasa.
Akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha kwa
mwaka 2013/2014 huko katika Baraza la Wawakilishi Chukwani,Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema sababu
kubwa ya kuvunjwa shirika hilo ni kushindwa kuhimili ushindani uliopo
wa biashara ya sekta hiyo.
Amesema kuwa taratibu za kulivunja rasmi Shirika la Utalii la
Zanzibar zinatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao kuanzia sasa.
Akizungumzia Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC) amesema linatarajia
kuweka vifaa vipya vya Studio pamoja na kununua gari moja ya kurushia
matangazo ya moja kwa moja kutoka nje ya studio hasa katika sherehe na
maadhimisho ya Kitaifa.
Waziri Said Ali Mbarouk amesema lengo la Wizara ni kusimamia
mazingira bora ya kazi ili kuliwezesha Shirika la ZBC kutoa huduma
bora na zenye ufanisi.
Akitoa maoni ya Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma wameshauri watendaji wa
Shirika la Utangazaji Zanzibar kubadilika kiutendaji. kufanyakazi kwa
umakini zaidi na kuacha kufanyakazi kwa mazoea .
“Kwa kuwa uendeshaji wa Mfumo wa Digital unahitaji umakini wa hali ya
juu kwa kutokuwa makini tutakuja kulaumiana na kuona ni bora
tungelibaki katika mfumo wa analogia”, alisema Mwenyekiti Mlinde.
Aidha ameeleza kuwa Utalii ni chachu ya maendeleo katika nchi jirani,
lakini bado Zanzibar haujapewa kipaumbele na kuwekewa mikakati na
kuwanufaisha wananchi wengi.
“Kamati inatoa rai kwamba dhana ya Utalii kwa wote itekelezwe kwa
vitendo na wala sio maneno pamoja na kuwekwa sera na sheria ambazo
zitapunguza gharama kwa wazawa.” Alisisitiza Mlinde.
Wameishauri Wizara kujidhatiti katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar
kwani kufanya hivyo utaweza kuongeza soko katika mataifa mbali mbali
na kuitangaza katika nchi za jirani.
Katika kutekeleza majukumu yake Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo imeomba iidhinishiwe jumla ya shilingi 9,985,000,000 kwa
kazi za kawaida na shilingi 510,000,000 kwa kazi za maendeleo.
Shirika la Utalii la Zanzibar limefanyiwa ufisadi kwa miaka mingi. Shirika linamiliki Mahoteli makubwa Zanzibar kama Bwawani, Afrika House, Zanzibar Hotel itakuwaje yashindwe na vihoteli mbuzi? Disco kila weekend linajaa, pesa zimekwenda wapi? Tupeni ukweli!!!
ReplyDeleteTatizo kubwa la shirika la utalii Zanzibar ni kutokusikiliza ushauri,
ReplyDeleteNilikuwa mmoja wa watafiti sekta ya utalii mwishoni mwa miaka 80s,na tuliishauri SMZ kuwa wangarifu na makini katika kufungua milango kwa wawekezaji wa sekta ya utalii,pia tuliwashauri wajipange na kujiandaa vema.
Jibu la mmoja wa maofisa wa juu wizarani alitujibu kuwa cha msingi kwa SMZ ni pesa za nje.
Sasa leo wanavuna walichopanda.
Mdau
Ughaibuni