Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration awamu ya pili leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Uingereza katika utekelezaji wa mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakiweka saini kwenye mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.Mradi huu unatekelezwa hapa nchini kwa ushirikia.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakionesha kwa waandishi wa habari hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration baada ya kumaliza zoezi la utiaji wa saini leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga akiwa na baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi wa International Inspiration wakimskiliza Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto alipokuwa akifafanua jambo baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mradi huu leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...