Na Mwandishi Wetu
SIYO siri, Julai 7, mwaka huu (Siku ya Sabasaba), anga lote la Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda wa saa 16. Burudani mfululizo pamoja na matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa, mengine ni adimu sana, yatachukua nafasi pana siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

Diamond.
Ni saa 16 za maajabu! Tafakari Mbunge wa Kigoma Mjini (Chadema), Zitto Kabwe, ataonesha uwezo wake wa kucheza masumbwi na kuchapana na staa wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi ‘Ray’. Je, ni vigumu kuamini? 
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, atakuwa na kibarua chake katika mchezo wa ndondi, atakapopanda ulingoni kuzipiga na malkia wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper. Uheshimiwa na usupastaa kando, zitapigwa ngumi tu kwa raundi nne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Zito wenzio wanapambana dhidi wa CCm we unafanya mzaha? anyway may be umeshajikatia tamaa ya URAIS ambao hata hivyo sijui nani alikudanganya kuwa watanzania tunakuhitaji uwe raisi wetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2013

    we mnyalu yako yanakushinda wataka vamia na ya Mh. Zitto...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...