Dada ambaye ni mwanasheria Bi Shamim Daudi akichangia maoni yake wakati wa Kongamano la wanataaluma wa Kiislam Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 1434 ambapo wanataaluma,  wanazuoni na taasisi zilitunukiwa zawadi na Pesa taslim.
 Wawakilishi wa Taasisi na makundi yalizotunukiwa Zawadi za kutambua Juhudi zilizotukuka katika kusukuma mbele juhudi mbali mbali za jamii ya Kitanzania.
 Ndugu Ramadhani Sanze Katibu Mkuu wa Baraza Kuu akifurahia baada ya kupokea zawadi kwa kuwakilisha taasisi za kiislam zilizoleta athari nzuri kiuchumi ndani ya Jamii ambayo ilikabidhiwa kwa SACCOS iliyochini ya Baraza Kuu iitwayo Kutayba ambayo hutoa Mikopo isiyo na Riba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Islamic Foundation akipokea Zawadi ya Kuwakilisha Taasisi zote za Kiislam zilizo mstali wa Mbele Kuelimisha Jamii kufahamu uislam na kujenga Taifa lenye amani na Utulivu.
 Mtafiti na Mtunzi Maarufu wa Historia za Kijamii Sheikh Mohamed Said (Wa Kwanza Kushoto) ni Mmoja wa Wanataaluma Wakongwe Waislam waliopewa zawadi na Umoja wa Wanataaluma wa Kiislam Tanzania kama miongoni mwa wasomi waliojitahidi Kuisadia Jamii wa Watanzania Kufahamu Historia sahihi ya Tanganyika.
 Dada Riziki Shahari akikabidhi zawadi ya uwakilishi wa wanawake wa kiislam wa kutolea mfano katika kuhamasisha jamii katika kujenga jamii yenye  Maadili na Manufaa kwa Mustakabali ya Taifa.
 Sheikh Jabir Katura wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Mwanza (Wa kati kati) alipokabidhiwa zawadi ya Kutambuliwa kama Miongoni Mwa Masheikh wenye Kusimamia mambo ya dini kwa Haki na Kwa Manufaa ya Jamii. Wakimkabidhi Zawadi hiyo Mwenyekiti wa Wanataaluma wa Kiislam Bw. Mussa Mziya (Kushoto) Pamoja na Mwenyekiti wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (Hay’at Ulaamaa) Sheikh Suleiman Amran Kilemile.
Mwakilishi wa Taasisi ya Islamic Help ya Uingereza Ndugu Shukuru Mohamed akikabidhiwa zawadi ya Kutambua taasisi hiyo kwa Mchango wake juu ya Watoto yatima katika Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2013

    Muumba awalipe kwa kuihudumia jamii

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2013

    Masha Allah, this is so courageous for the Muslim Umma. May Allah reward you the most of what ever you do Inshaa Allah.

    ReplyDelete
  3. Fatma SalimJuly 12, 2013

    Mashaallah, Mungu afanye liwe jambo la kudumu. Ni jambo jema kuonyeshana mapenzi wakati tupo hai kwani inahamasisha.

    ReplyDelete
  4. Saleh SalimJuly 12, 2013

    Good Initiative, just need more awards to cover all over the Country Muslim Reliable and Dependable leaders not Corrupted who eats Muslims properties.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...